Swali la kwanza linahitaji ufafanuzi zaidi, hizo PC zipo connected kwenye switch au? na internet zinapataje? kutoka kwenye modem au kupitia hiyo main PC? Pia ukiweka hizo settings kwenye PC nyingine haikubali?
Kuhusu kuconect automatically.
Kwanza hii Modem inauwezo wa kuconnect yenyewe bila kutumia PC mfuate huyu bwana YouTube - how to make your fawri modem smartAx Mt880 router na maelezo yake, sijui ni lugha gani hii ila inaeleweka ukifuata steps, kama TTCL wamezima option hiyo basi fuata maelezo yangu. Pia YouTube - Make Fawri Router & Autoconnect
Ikishindikana ya kwanza fuata hii.
Ninavyoelewa ni kwamba kukonect na internet inabidi u-log in kupitia Windows si ndio? Kama ni hivyo:
Nenda control panel Network connection.
Itafute connection yako ya TTCL.
Right click nenda properties.
Toa ticki kwenye "Prompt for name and password..."
Click ok.
Right click connection tena, nenda Create shortcut.
I move hiyo shortcut had kwenye Startup folder in XP nadhani ipo
C:\Documents and Settings\All Users\Start Menu\Programs\Startup
Sasa intenet yako itaconnect PC ikistart.
Kuhusu kublock sites unaweza kuinstall blocking software kwenye PC zote mfano Naomi - Free software downloads and software reviews - CNET Download.com, au kutegemea na unaitumia vipi hiyo main PC kama server? Unaweza ukablock hapo kwenye main PC yako kama connection zote zinapitia hapo so kama unatuitumia kama Proxy server, inaweza ikawa na option ya kublock sites either manually au automatically.
Mwishoni unaweza kutumia service kama OpenDNS wana option ya blocking sites za makundi fulani, so utaset network yako itumie DNS zao and then itablock kutokana na domain name.