Huwa najiuliza,nyie wanawake mnadai haki sawa,kuna eneo sijasikia mnalizungumzia liondoke,suala hilo ni kuwa;Mwanamke anapoolewa kwanini anabadili ubini?Hii si inakua kama "Umemilikiwa"?Unakuta anaitwa Lydia James Rweyemamu,akiolewa na John Bernad Mushi,anaitwa Mrs Mushi au Lydia Bernad Mushi,Why?Au eneo hili kwenu ni poa?
sio wote wanabadili, kama mimi sijabadili na wala sina huo mpango...
Ukiolewa utabadili?Na unapobadili unakua unamaanisha nini?Na unapoacha je?
watoto je ? Ngoma mzito
Ka swali kazuri!
Sasa Eiyer ndugu yangu, mtoto nimtoe tumboni mwangu mimi mwenyewe, nimpe jina kwa ubini wangu mimi mwenyewe, baba atatambulika kweli?? Mimi mama ninajulikana kwa sababu ndie niliemtoa mwanangu tumboni, wewe baba je?? Just thinking........lakini sio mbaya mama akimuita mwanae jina lake.
Sometimes unampa mtoto jina lake-la ukoo wa mama-la ukoo wa baba.(mfano: amina (jina lake mwenyewe)-Hamadi (jina la ukoo wa mama, badala ya jina la baba)-Sharif (jina la ukoo wa baba)Sasa Eiyer ndugu yangu, mtoto nimtoe tumboni mwangu mimi mwenyewe, nimpe jina kwa ubini wangu mimi mwenyewe, baba atatambulika kweli?? Mimi mama ninajulikana kwa sababu ndie niliemtoa mwanangu tumboni, wewe baba je?? Just thinking........lakini sio mbaya mama akimuita mwanae jina lake.
Kama mtoto umembambikia jina linamaana?
Jina kitu kidogo, kwani tukibadili tunabadilika nin? Sisi tunalilia usawa katika mambo ya muhimu na ambayo tukiyakosa yanaweza kuleta impact kwa namna moja au nyingine katika maisha yetu.