Mambo mengine kuyatetea ni upuuzi mtupu.
Inchi zote zinazojitambuwa huwezi kukuta abiria wanapanda mabasi uchochoroni.
Ni Kwa vile serikali yetu inaendeshwa Kwa mihemko ya mitandaoni.
Ni wakati sasa wa mabasi yote yawe sehemu moja.
Hii itapelekea watu wote hata wageni kutambuwa sehemu maalum ya kupata usafiri.
Muhimu ni kuwa na connection za usafiri kutoka pembezoni mwa mji kufika Magufuli terminal.
Wabongo tupunguze uswahili na ujuaji usio na msingi.
Mbona JNIA airport watu wanafika na kuondoka kwenda makwao bila kulalamika?
Mbona hawasemi airport isogezwe karibu na kwao.
Vitu vingine ni upuuzi mtupu kulalamika.