Mtoto wangu alizaliwa akachelewa kulia, hadi sasa shingo haijakaza na bado hajaweza kukaa vizr! Ana miez 9. Hv kuna uwezekano wa kukua vzr kama watoto wengine? Naomba msaada
Pole sana kaka Elias....hiyo condition inaitwa 'Cerebral Palsy'. Moja ya sababu zake ni kama uliposema wewe kuwa mtoto alizaliwa akachelewa kulia. Mtoto anapozaliwa anapaswa alie immediately, hii inamsaidia kupanua mapafu na kuweza kupumua, hivyo basi damu yenye oksijeni ya kutosha kuufikia ubongo wake mchanga mapema na kuweza kuanza kazi mapema.
Mtoto hasipolia (mara nyingi inasababishwa na kuchoka kutokana na labor kuchukua muda mrefu kupita kawaida), anachelewa kupanua mapafu na kupata oksijeni ya kutosha kwenda kwenye ubongo sehemu ya Cerebrum, na hii husababisha permanent damage kwenye ubongo wake mchanga. Na hili husababisha matatizo katika ukuaji wake kiakili (mental) na kimwili (motor). Na ni bahati mbaya sana kuwa 'hakuna tiba tatizo hilo'.
Ni dhahiri kuwa mwanao hataweza kukua kama watoto wengine wa umri wake, atakuwa analag behind maisha yake yote, na pengine kwenye severe cases (nadhani hii ya mwanao ni mojawapo) mtoto anaweza pata ulemavu wa viungo kukakamaa (Spastic quadriplegia kama itahusisha miguu na mikono yote, au Spastic hemiplegia kama itahusisha mikono tuu au miguu tuu au mguu na mkono).
Hata hivyo, kuna mambo kadhaa unaweza fanya kumsaidia mtoto katika ukuaji wake. Kuna clinic maalum kwa ajili ya watoto wenye Cerebral Palsy Muhimbili idara ya watoto, hapo utapewa elimu ya jinsi ya kumtunza mtoto mwenye tatizo hilo, na utakuwa unampeleka mara kwa mara kutokana na ratiba utakayopewa kwa ajili ya ufuatiliaji. Pia hapo baadae kuna shule maalum kwa ajili ya watoto wenye tatizo hilo ambapo kuna walimu specialized wa kuwafundisha. Naifahamu moja iko Ifakara inaitwa 'Bethlehem Centre'.