Hiari yenye hamasa

Hiari yenye hamasa

hafidhasha

Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
18
Reaction score
19
Hiari yenye hamasa, ni nini maana yake?

Ni kutenda badala ya kusema, si kusema nitafanya ila ni kutenda na kuwa mfano.

Ni kuamua kuwa mfano chanya kwa familia yako, rafiki zako, watu wanaokuzunguka, unaowajua na usiowajua.

Ni kuamua kuibadilisha dunia kuwa bora kuliko ulivyoikuta.

Ni kujitahidi kadri ya uwezo wako kubadilisha mambo hasi katika jamii kuwa chanya.

Ni kuamua kuishi kwa kufuata kanuni “kuwa proactive na sio reactive”.

Usijidanganye, matatizo unayokutana nayo sio adhabu bali ni zawadi, kwani yanakuandaa kuwa mtu unaestahili na unaeweza kuhimili ushindi unaokusubiri.

Aliniambia Baba, “Mwenyezi Mungu ametuumba wanaadamu kuja kuwa makhalifa katika dunia, hivyo sasa, jenga kasri yako popote ulipo, haijalishi upo katika mazingira gani, tulishapewa ushindi na uwezo wa kufikia malengo yetu na mwenyezi, lililobaki ni sisi kuamua kupambana kufika tunapopataka, na haya yote huanza akilini.

Hakuna silaha yenye manufaa kama akili iliyo chanya, itafungua milango ambapo wewe ulidhani pana ukuta.

Imarisha mawazo yako kwanza, kuwa na akili chanya, mengine yote yatakaa sawa”

Usikubali kupita duniani kama upepo, jenga alama yako, ili ukiondoka uwe umeizawadia dunia, watu wakikukumbuka wapate tabasam usoni mwao.
 
Back
Top Bottom