Hidaya Kutoka Kwa Sheikh Suleiman Takadir

Hidaya Kutoka Kwa Sheikh Suleiman Takadir

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA ADIMU ZA SHEIKH SHULE TAKADIR ALIZOACHA BAADA YA KIFO CHAKE 1958

Leo nimepokea picha mbili kutoka Zanzibar kwa mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir, Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir.

Miaka 66 imepita na toka Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alipofukuzwa TANU mwaka wa 1958 na akafariki mwaka wa huo huo wengi wakiamini kwa msongo wa mawazo.

Historia ya Sheikh Suleiman Takadir na ugomvi uliotokea baina yake na Rais wa TANU Julius Nyerere hauhitaji kuelezwa kwani sasa ni historia mashuhuri.

Halikadhalika kama Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kakosea kwa yale aliyosema hili liko wazi na mbele yetu kufanyiwa tathmini na kulizungumza.

Picha ya kwanza ni hiyo inamuonyesha Sheikh Suleiman Takadir amesimama na Julius Nyerere ni wa tatu amekaa akifuatutiwa na John Rupia.

Ukiangalia kwenye meza iliyo mbele ya Sheikh Suleiman Takadir utaona kuna kikapu cha ukili na bakora.

Bakora hii ina historia kubwa sana katika historia ya TANU.

Hii ndiyo bakora Sheikh Suleiman alimnyooshea Julius Nyerere na kusababisha mtafaaruku mkubwa uliosababisha yeye kufukuzwa TANU na kufutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Picha ya pili ni hiyo Sheikh Suleiman Takadir anaonekana akiwa bila shaka katika dhifa.

Kulia wa pili ni Sheikh Suleiman Takadir na wa pili kushoto ni John Rupia.

Sheikh Suleiman Takadir kupitia picha zake alizoacha leo anazungumza na sisi kutoka kaburini.

Hii kwa hakika ni hidaya kutoka kwake kuja kwetu.
 

Attachments

  • Screenshot_20241011-140716_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20241011-140716_WhatsApp.jpg
    87.6 KB · Views: 8
  • Screenshot_20241011-122505_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20241011-122505_WhatsApp.jpg
    85.3 KB · Views: 12
Bakora hii ina historia kubwa sana katika historia ya TANU.

Hii ndiyo bakora Sheikh Suleiman alimnyooshea Julius Nyerere na kusababisha mtafaaruku mkubwa uliosababisha yeye kufukuzwa TANU na kufutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini tukiangalia picha ya pili mboni bakora imeshikwa na John Rupia hii maana yake kwamba bakora hio haikua bakora ya Shekhe?
 
Back
Top Bottom