Hii biashara imenichanganya

Hii biashara imenichanganya

wiseboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
2,930
Reaction score
3,305
hbr jaman....
kuna sehem nategemea kupata 6m sasa nilitaka kuweka kwenye broilers sasa mahesab mbona yanaleta lost

kwa kuku
mmoja
Wiki ya 1 15g*kuku 1000=15,000 sawa na kilo 15kwa siku na sawa kilo 105 kwa wiki na ni sawa na mifuko 2 ya chakula (2bags@50,000/ )
=100,000

Wiki ya 2 25g *kuku 1000=25,000 sawa na kilo 25kwa siku na sawa kilo 175 kwa wiki na ni sawa na mifuko 4ya chakula (4bags@50,000/ )
=200,000/

Wiki ya 3 35g *kuku 1000=35,000 sawa na kilo 35kwa siku na sawa kilo 245 kwa wiki na ni sawa na mifuko 5 ya chakula (5bags@50,000/ )
=250,000/-

Wiki ya 4 50g *kuku 1000=5000 sawa na kilo 50 kwa siku na sawa kilo 350 kwa wiki na ni sawa na mifuko 7ya chakula (7bags@50,000/ )
=350,000/-

Wiki ya 5 65g *kuku 1000=65,000 sawa na kilo 65kwa siku na sawa kilo 455 kwa wiki na ni sawa na mifuko 9 ya chakula (9bags@50,000/ )
=450,000/-

Wiki ya 6 85g
*kuku 1000=85,000 sawa na kilo 85kwa siku na sawa kilo 595 kwa wiki na ni sawa na mifuko 12ya chakula (12bags@50,000/ )
=600,000/-

Wiki ya 7 105g *kuku 1000=105.000 sawa na kilo 105kwa siku na sawa kilo 735 kwa wiki na ni sawa na mifuko 15 ya chakula (15bags@50,000/ )
=750,000/-

Wiki ya 8 120g *kuku 1000=120,000 sawa na kilo 120 kwa siku na sawa kilo 840 kwa wiki na ni sawa na mifuko 17 ya chakula (17bags@50,000/ )
=850,000/-

JUMLA YA GHARAMA YA CHAKULA NI 3,550,000 PLUS GHARAMA YA KIFARANGA KIMOJA 1500 sawa na 1,500,000/ inakuwa jumla 5.5m
sasa ukaja kuuza kwa 5000 si ni sawa na 5m bado sijaweka gharama za dawa ....mhudumu...transport cost tuseme inafika 6m sasa hapa ni biashara au hasara? je mnaofanya hii project nyie mnaifanyaje kupata faida? mbona mm nachemka
 
huo mchanganuo hapo juu umeangazia hasa chakula kwan ndo kibatumia hela nyingi kwenye biashara ya kuku.......sasa kwa hawa kuku miez 2 najua kitaalam inabidi wale kama ifuatavyo

kiwango cha chakula kwa kuku wa nyama kwa siku
wiki ya kwanza= gram 15
wiki ya pili =gram 25
wuki ya tatu= gram 35
wiki ya nne= gram 50
wiki ya sita = gram 65
wiki ya saba=gram 85
wiki ya nane= gram 105
sasa kwa kutumia hii kwenye chakula ukifanya hesabu kwa wiki ndo unapata hiyo hesabu hapo juu
 
Nafikiri pia mchanganuo wako hauko sawa kwanini uwauze at 8 weeks? sijafanikiwakufuga wengi hivyo ila nami nawafuga. 400 wanakula mifuko 24 mpaka nimalize kuuza. Bei ya kununua ni 400*1400 = 560,000 chakula 24*50,000= 1,200,000. matumizi mengine maji umeme kijana dawa( glucose+ booster) total naweza tumia 150,000/-

Matumizi yote ni 560,000 + 1,200,000 + 150,000 = 1,910,000.
Mauzo 6,000*400= 2,400,000/- huwa napata faida between 350,000 - 450,000 na ikitokea zali nikauza kwa 6500 well then faida juu.

Ila biashara hii yataka moyo si ajabu kukuta kuku 30 wamelala asubuhi wakati usiku wote walikuwa poa
 
asante Mom basi hii biashara haina mzunguko wa faida..ina maana laki tatu nusu as faida ukigawanya siku 44 ambayo ni ndo hizo wiki 6 unakuta kwa suku ulikuwa unahangaikia faida ya 7000/- dah na kuku wanavyosumbua vile..mhhh hapana
 
Last edited by a moderator:

We unaona hiyo Faida ndogo,kwani hiyo milioni sita ni kubwa?
We kaa nayo miezi mitatu ndani ndio utajua.
Siku hizi hakuna biashara yenye faida kubwa kama unavyofikiria,na wala hakuna biashara ya kuzemebea,lazima ujikaze mtoto wa kiume.
Anaesema anajenga kwa ajili ya mifugo ujue ananidham yapesa ya hali ya juu,sasa wewe wastan wa mwezi unaingiza pesa hiyo,na baadhi ya siku inazidi hapo hadi laki 4.Hapo umekosa nini.
La sivyo,nunua bodaboda ukajimalize,maana kwa ulivyo huko ndio kutakutoa roho.Biashara uvumilivu kaka
 
Kweli watu wamejenga kwa kufuga kuku kama alivyosema spices kunahitaji nidhamu ya pesa ya hali ya juu na hawakujenga kwa siku moja, tatizo vijana wanataka watajirike ndani ya mwezi mmoja kitu ambacho sio sahihi,m6 ni mtaji wa kuku 1000 ambao ukifuga bila matatizo unaweza pata faida ya zaidi laki 8 ndani ya wk 4-5.
Inapaswa tujifunze kufanya biashara inayokua anza kuku 500 baadae ufike kuku laki moja, kutajirika ni safari ndefu.
 
We unaona hiyo Faida ndogo,kwani hiyo milioni sita ni kubwa?
We kaa nayo miezi mitatu ndani ndio utajua.
Siku hizi hakuna biashara yenye faida kubwa kama unavyofikiria,na wala hakuna biashara ya kuzemebea,lazima ujikaze mtoto wa kiume.
Anaesema anajenga kwa ajili ya mifugo ujue ananidham yapesa ya hali ya juu,sasa wewe wastan wa mwezi unaingiza pesa hiyo,na baadhi ya siku inazidi hapo hadi laki 4.Hapo umekosa nini.
La sivyo,nunua bodaboda ukajimalize,maana kwa ulivyo huko ndio kutakutoa roho.Biashara uvumilivu kaka

duuuuuh sijaelewa umenipa madongo au ushaur
 
Namia naomba ushauri wenu, nigependa kuaanza hii biashara na kuku si zaidi ya 100, zumuni la kuaza ni kutunza saving yangu ili iweze kuongezeka japokuwa kwa kupata faida kidgo ni bora kuliko kuitunza,bank na kila mwezi kulipa service fee kila mwezi
 
Mie naanza next mouth na chotara 100, hope nitakuwa nawapatia update kupitia jukwaa hili coz nilipata idea hiyo hapa hapa na nimefanya utafiti kidogo since july na pia nimewatembelea wafugaji kadhaa kujua wao wamefikaje hapo walipo ikiwemo kusoma majarida kazaa walionipatia.
 
Hizi hesabu zako nadhani zipo too theoretical , mimi nafuga broilers kwa week4-5, hesabu yangu ya total expenditure ni 350,000-370,000 kwa kila kuku 100 na total turnover ni 100'000-130'000. Hii calculator haijawahi kuniaibisha
 
Mkuu Ontario nisaidie kuku unauzia wapi? Kwa bei gani? Nitashukuru ukiniPM namba za wateja wa broilers
 
Nafikiri pia mchanganuo wako hauko sawa kwanini uwauze at 8 weeks? sijafanikiwakufuga wengi hivyo ila nami nawafuga. 400 wanakula mifuko 24 mpaka nimalize kuuza. Bei ya kununua ni 400*1400 = 560,000 chakula 24*50,000= 1,200,000. matumizi mengine maji umeme kijana dawa( glucose+ booster) total naweza tumia 150,000/-

Matumizi yote ni 560,000 + 1,200,000 + 150,000 = 1,910,000.
Mauzo 6,000*400= 2,400,000/- huwa napata faida between 350,000 - 450,000 na ikitokea zali nikauza kwa 6500 well then faida juu.

Ila biashara hii yataka moyo si ajabu kukuta kuku 30 wamelala asubuhi wakati usiku wote walikuwa poa

Mkuu Mom msaada kwenye tuta, hiyo naonba uniunganishe na wateja wako wa kuku. Hao wanaonunua mmoja kwa elfu 6. Natanguliza shukran
 
  • Thanks
Reactions: Mom
Nikirudi kwa mleta uzi Wiseboy, ushauri alikupa Zanzibar Spices nakubaliana nao. Kila mtu.ana staili yake ya kushauri. Nami najenga frame za biashara kwa biashara hii hii ya kuku broilers. Ingawa napata changamoto ya kulaliwa bei ya kuku at the end of the day. Ila sikati tamaa wala siachi kufuga. Kwanza kabisa huo.mchanganuo wako si wa kweli. Bado hujafanya research vzr. Bei ya juu ya kifaranga ni 1400, interchick. Nimenunua leo vifaranga vya Mkuza kwa 1000/-. Chakula cha kuku ninachotumia hakizidi elfu 43. Kuku wanauzwa kuanzia wiki ya 4-5. Kwa sasa huwa naweka kuku batch 2, elfu 1 vifaranga na elfu 1 wakubwa. Ila nilianza na kuku 400 na walikuwa wanatumia mifuko km 26. Mahesabu ya Mom nakubaliana nayto. Fanya hesabu km kuku 400 mifuko 24, kuku 1000 mifuko mingapi. Na pia kutokana na soko wakati mwingine ni changamoto, kwa wewe unayeanza sikushauri uanze na 1000. Anza angalau na 500
 
Hizi hesabu zenu bado zinanipa shida sana mkuu..

Ila nashukuru sana kwa maelezo yakinifu mliyoyatoa tw Zanzibar Spices na Mom
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mom msaada kwenye tuta, hiyo naonba uniunganishe na wateja wako wa kuku. Hao wanaonunua mmoja kwa elfu 6. Natanguliza shukran

niko mkoani huku hiyo ndiyo bei general na kuku tunauza between 5-6 weeks. kwa Dar nimeona bei ni 5000 kutokana na kuwa mnawauza at 4-5weeks so hata chakula hakitumiki kingi kama anayefuga mikoani.
 
Back
Top Bottom