Hii Chuki inatokana na nini? Hili jambo limeusononesha moyo wangu

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Mmoja ya madereva wetu amepatwa na shida kidogo ya kifamilia. Nikaona ni vyema kumtembelea jamaa huyu sababu namfahamu kitambo kabla hajawa dereva wa ofisini.yeye ndo alishiriki vizuri sana kunifundisha kiswahili miaka hiyo nafahamu kiingereza, kichina, kijerumani na kihispania.

Nimeenda mitaa anayoishi Masaki. nimeshtuka leo naendesha gari nawaona ducks. niliambiwa wanaitwa bata.kiuhalisia hawa nimekuwa nikiwaona tu kwenye movies na picha.

Basi kumbe wakati naondoka baada ya kuwaangalia na kupiga picha waliingia chini ya gari...sina hili wala lile nikakanyaga wawili.

Raia walipiga kelele mpaka mmoja kunikimbiza na pikipiki.mimi nilikuwa kwenye Merc Benz kama kawaida nimefunga vioo vumbi lisiingie.ndio anakuja kupark mbele yangu.nikamwuliza shida nini.akajibu nimeua bata.

Kiukweli hili liliniumiza moyo sana.nilimwomba turudi mpaka sehemu husika.haikuwa mbali kwenda nikakuta jamaa wamewawahi kuwachinja kabisa.

Basi nikauliza utaratibu unakuaje.ndio kunambia kuwa kwa wale bata wadogo kila mmoja natakiwa nilipe tsh 70,000. Nikatoa 300,000 nikawapa.na yule dereva wa boda boda aliyenifuata nikampa 50,000 ya usumbufu na mafuta.ingawa umbali toka sehemu ya tukio na aliponikuta ni kama hatua 30 tu.

Shida ilikuwa maneno magumu jamaa waliyoyatamka wakishutumu kuwa wenye magari wanadharau sana hawajali watu wengine tena mmoja akasema nilipopita hata sikuwasalimia.

Nilishangaa kusema nyie wenye vijihela mna jiona bora leo sasa ndo utatuelewa sisi nasi maeneo yetu.wengi walionekana kuwa na hasira ambazo sielewi zilitokana na nini.kijana mmoja tu ndio alionesha uungwana na kuwaambia mbona sikuwa nimeongea neno lolote baya.

Huyu alionekana kuwa na uwezo mzuri wa kureason.nilimwachia 50,000 aweke voucher anitafute siku moja tuongee.

Sifahamu kwa nini watanzania wengi wanapomwona mtu mwenye kauwezo kidogo wanamwona ni adui.hili nimeliona sehemu nyingi sana.wakisikia kuna mtu kafilisika wanafurahi.

Hawaangalii kwa kufilisika huyu wangapi watakosa ajira.kama nikiuza magari yangu au yakifa hawaoni kuwa mafundi wa dt dobie na cfao watakosa kazi? Je vituo vya mafuta vya total sisi wenye magari wote tukawa hatuna magari nani atanunua mafuta lita 60 na zaidi kwa week?hivyo kuna watu watakosa kazi.

Wanapokuwepo wenye pesa mzunguko unakuwa mkubwa.unadhani ukiniombea mabaya nikiacha kwenda supermarkets kubwa kubwa wale waajiriwa nani atawalipa?

Haya mambo yanategemeana sana kama hujaajiriwa direct na mwenye pesa unaajiriwa indirect.lakini ni wangapi tunasaidiana mfano gari zangu zote sita sasa ( nimeingiza Jeep last week) unadhani nani anaosha?

Anyway tusiombeane mabaya ndugu zanguni. Mimi nauza FORD RANGER unadhani kama wote ni makapuku nani atanunua? Si gari itaozea tu parking kwangu?

Kuna siku nilijisikia vibaya nipo sehemu nina FORD RANGER pale posta nimepark zile parking za Golden Tulip naenda nakuta kuna mtu mwingine pia anayo gari hiyo hiyo na Rangi zimefanana. Ndio siku niliyoamua kuiuza.

Nashukuru kuna Jamaa ofisini kanambia anaihitaji maana anadai ni kama imetoka Japan leo hii hii. Imetembea kms chache kwa maneno yake 38,000. Tyres mpya n.k

Tuishi kwa upendo nikipata mimi shukuru.na ukipata wewe nitashukuru.unadhani ningefanya nini hii gari kama ndio mimi peke yangu nina pesa wengine ndio hivyo tena?

Sisi wenye vijicent tunapenda tuwe wengi ili biashara zetu ziende vizuri maana nikiwa peke yangu kuna mambo nitakwama.tuache kuchukiana isipokuwa tuombeane mema.

Maneno ambayo walisema jamaa yalikuwa ya kusononesha sana walionesha chuki kwangu wakati sijafanya kosa lolote.
 
Hiyo ni Dunia nzima, labda kama haujawahi kutembea, kuna uadui mkubwa kati ya wenye magari vs baiskeli na watembea kwa miguu, ni Dunia nzima siyo kwetu tu.
Kwanza Ulaya hata watembea kwa miguu/baiskeli wameanza hata kuchoma moto wenye magari hasa SUV!
 
Japo kama kawaida yako umejijaza misifa lakini ujumbe mzuri.

Maskini tunaamini matajiri ndio chanzo cha sisi kuwa hivi tulivyo.😀😀

Tunaamini matajiri wote watateseka motoni.😀😀

Tunaamini matajiri wana dhambi sana kuliko sisi.😀😀

Siku tukiachana na haya mawazo ya kujinga tukaamua kujifunza huenda umaskini wetu ukapungua au kuisha.
Hayo mawazo ndio hufanya akili zetu kudumaa.
 
Aisee kbla ya yote n kwel chuki zipo tena sana kwa sisi wa kipato cha chini na sijui shida huanzia wap
 
Na hii dhana inafanya mpaka mtu fulani akitumbuliwa watu wanashangilia as if mafao yake yataletwa pale kijijini watu wanywe soda.
 
Hakiamungu leo nimeamini huyu bwana kiduku anayoyahadithia hapa ni ya kweli kabisa sikuwahi kuwazaga. Mi ni shuhuda wa tukio zima jinsi alivyowagonga bata mpaka amefukuzwa na kulipa fidia yote. Nilkua nimevalia pensi nyeusi na flana ya kahawia sikua nafoka kama wengine nilkuwa kimya tu.
 
Kapicha vipi hukupiga?
 
Nyinyi vijana hamuelewi kinacho endelea.
Uchumi na maendeleo ni sanaa Art ni vision maono ya mtawala.
Majibu au matokeo ni positive au negative.
Yanaweza kuumiza watu na wakajenga chuki bila sababu.
Mkubwa alisema waishio kama malaika wataishi kama mashetani, tukakenua meno.
Majibu nihayo sasa watu wanachuki iliyo pandikizwa.
Wafanya biashara ni maadui wakubwa kwa watawala.
Mara kangomba mara matapeli utadhani wamewapa mitaji.
Matokeo watu wanaogopa kufanya biashara mara ushuru kodi soko hakuna unafilisiwa.
Atakayenunu mazao ya mkulima ni nani??
Badara ya kuhasisha unadhulumu vitisho na kufilisi.
Mabenki hoi maduka yanafungwa, watu wanakimbia hovyo, upendo utatoka wapi watu wana njaa.
Bei ya mbaazi kijijini bei ni Tshs 50,000/= wakati ilikuwa Tshs 300,000/= Kwa gunia kina Dewiji wamekimbia. Sijui mazao mengine, vitu bei iko juu haishuki.
Utachekewa na nani na benzi lako mtaani, fikilia!!
 
Ukiwa na pesa kifua kinajaa kujiamini na amani,

Lakini ukiwa masikini kifua kinajaa chuki na kutokujiamini, kuhisi kila anayekuona ana kudharau.

Tiba ni moja tu, kutafuta pesa kwa nguvu na akili zote.

Hata sisi wenye Gutta zetu kuna watu tukipita barabarani wana tununia weeeee utafikiri tuliwapora kiwanja cha urithi.
 
Kiduku Lilo,

Pole sana. Hili ni tatizo la hapa Tanzania, hasa kwa mtu ambaye hajabahatika kuona ufanisi wa mtu mwingine unavyomhusu na yeye binafsi. Ni ile dhana ya tukose wote. Lakini dhana hii ilikuwepo katika historia ya uelewa hapa duniani. Dhana yenyewe ilikuwa inajulikana kama "the two zero sum game" maana yake ufanisi wa mwingine lazima upunguze ufanisi wa mtu wa pili, tofauti na dhana ya "win win" yaani uwezekano wa mtu mmoja anayefanikiwa kumfanikisha na mtu wa pili.

Jinsi watu wengi wanavyokuwa kwenye dhana hii ya pili katika jamii ndivyo maelezo yako uliyotoa yatakavyoeleweka kwa urahisi na yakawa mambo ya kawaida. La kusikitisha, hao ambao wanachukia mtu mwenye vijisenti hawajishughulishi kujiuliza mwenzao alivipataje hivyo vijisenti; wao jibu lao ni rahisi tu, "Mwizi huyo" kumbe pengine badala ya kuleewa pombe au wanawake, yeye hivyo vijisenti aliwekeza kwanza; au pengine mwanzoni alifanya kazi bila kulala usingizi kama wao walivyofanya.

Na Serikali yetu wakati mwingine ilichangia kwamba mtu ambaye ana biashara au shughuli binafsi ni "mwizi". Ndiyo maana hapo awali mwanachama wa TANU/CCM alitakiwa awe ama mfanyakazi au mkulima! nje ya hapo hupati kadi wakati huo! Huko ndiko tunakotoka. Itatuchukua muda kidogo kufikiri kisasa.

Itachukua muda kidogo pia kwa sababu ya aina yetu ya elimu kwa sababu hata waliosoma hivi karibuni wengi wao wanafikiri hivyo hivyo. Wanafurahia mtu anapoangushwa au kutumbuliwa hawajali kama anafanyiwa hivyo ki makosa au kwa uhalali. Itachukua muda kidogo kutoka hapa tulipo. Tafadhali tuvumilie.Mwisho wa yote, pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…