Hii dhana kwamba walimu hawazeeki ina ukweli wowote?

nakwede97 pale juu kasema wanaishi kwa nidhamu sana kwa sababu wana kipato kidogo na wewe hapa unasema hawaonekani kuzeeka kwa sababu ya kipato cha uhakika. Jibu sahihi ni lipi?

nimeongelea kihistoria maana yake zamani miaka ya themanini huko siku hizi ofcourse hiyo theory yangu haina uhalisia tena hasa mijini lkn zamani walimu ndiyo watu waliokuwa na ajira ya uhakika ingawaje ndiyo mishahara ilikuwa midogo lkn bado walikuwa na uhakika wa mwisho wa mwezi hela kuingia.

ukienda vijijini hili hata leo unaweza kuliona middle class huko vijijini ni walimu wao ndiyo wanye uwezo wa kununua vitu, kupanga chumba hapo kijijini na wengine wenye uwezo pia ni manesi kama hicho kijiji kimebahatika kuwa na zahanati, hata leo ni hivyo huko vijijini ...
 
Simple tu maisha yao ni magumu kinyama, wanashindia mihogo na viazi , wanatembea umbali mrefu kuepuka nauli za pikipiki na bajaj sasa kisukari na pressure wanakipata saa ngapi? Ukienda TRA utakuta nido , jam na makorokoro mengi walimu chakula Chao cha kwanza ni saa 8 akitoka job, jaribu na wewe hutozeeka
 
Mimi nina maisha magumu kuliko walimu lakini mbona nazeeka 🀣
 
Nadhani hii inawahusu pia watu wa afya pia hasa wauguzi maana nao kazi zao zinahusisha kutembeatembea, watu wa kwenye majeshi pia walitakiwa ndio wawe wanaongoza kwa 'kutokuzeeka'. Kwa nini walimu tu?
Well, kingine ni suala zima la Ulevi na ulaji, Wanajeshi wanaishi muda mrefu sababu ya mazoezi na walipaswa wawazidi Waalimu, ila mie naona kama Wanajeshi wamalizwa zaidi na Pombe wanazokunywa kupita kiasi na magonjwa yanayoambatana na pombe hizo
Ukikuta Mwalimu mlevi kupita kiasi ni nadra sana kwsbb anapaswa kudamka mapema kuingia class halafu na codes of Conduct au Haiba ya Ualimu inamfanya aogope kufanya mambo flan flan km kulewa sana...kwa Majeda hilo halipo
Ni mtazamo wangu mie lakini 🀣Lifestyle ndio sababu
 
Asante kwa maelezo mazuri mkuu
 
Ni kweli aisee, mwl anayefanya kazi yake kwa wito ameridhika 100%

Stress za kutaka kuwa matajiri zinatuzeesha fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…