Juzi kati nimetulia bar moja kwa Morombo, sasa kuna jomba mmoja alikua anakunywa K-Vant kumbe jamaa kichwa panzi!
Akaanza kumzingua bar maid Mara, arushe matusi. Sasa kuna majomba yalikua yamekaa pale kaunta yametulia tu yanashusha mtungi mdogo mdogo kimya kimya
Yakamuita yule bar maid yakamuuliza yule duanzi anakunywa bia gani akajibu Serengeti
Wakamuambia mpe yule duanzi kreti moja ya serengeti alafu muambie atoe jam hapa na asirudi leo tena hapa
Sister kampelekea jamaa, jamaa anashangaa shangaa🤣
Wakamuambia aupokei au?
Jitwishe kreti nenda zako na leo usirudi hapa
Jamaa akajitwisha akang'oa zake😂