joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Hivi inawezekanaje nchi yenye jeshi, POLISI, na vyombo vingine vya ulinzi, lakini bado kuna watu wanasema hadharani kwamba wao ndio serikali na hawaitambui serikali iliyoko madarakani na bado hawachukuliwi hatua?.
Kazi muhimu na msingi ya serikali yoyote duniani ni kudhibiti usalama wa raia wake, wajione salama popote pale walipo, serikali yoyote inayoshindwa kutimiza wajibu wake huo wa msingi, ni serikali iliyoshindwa " Failed state".