Hii hapa Ndinga ya Wolper iliyogharimu milioni ishirini

Hii hapa Ndinga ya Wolper iliyogharimu milioni ishirini

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
750
Reaction score
656
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake.http://husseinjuma.blogspot.com/2016/11/hii-hapa-ndiga-ya-wolper-iliyogharimu.html
========

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake

Ijumaa lilimbabatiza Wolper mitaa ya Kinondoni jijini Dar akiwa na gari hilo aina ya Toyota Alphard ambapo alipobanwa kama amelikodi kama wanavyofanya mastaa wengine au amenunua alifunguka kuwa ni lake kutoka kwenye hela yake halali.

“Hii gari ni yangu kama mnavyoiona mpya kabisa, nimeinunua na ndo’ kwanza nashughulikia usajili,” alisema Wolper.

Wolper alisema kuwa anakwepa mambo yaliyompata kwenye ile gari yake iliyomletea matatizo aina ya BMW X-6 ambapo alipata funzo na sasa hawezi kufanya makosa

“Nimeamua nifanye usajili kabisa TRA, sitaki matatizo kabisa kuhusu magari, lile lilinifanya nipate funzo kubwa,” alisema Wolper.

Wolper mbali na kununua gari amefungua duka la nguo Kinondoni. Kufuatia mambo hayo makubwa aliyofanya msanii huyo, wadau walihoji kama mkwanja wa kufanyia yote hayo umetokana na safari ya China au kuna pede

CHANZO: Ijumaa
 
Hawa wasanii wetu ni noma kwa kupenda sifa.hii gali ukiagiza Japan be forward inafika hapa kwa 10,000,000/tzshs.kuinunua hiyo ni $800
 
mi nimeishia kusoma heading tu..hiyo link nimegoma kufungua....maana huo ni ufwala!
 
Atakua ameinunua kwa hela alizopewa na ccm alipojiunga nao. Otherwise kwa kuuza ....... asingewezaununua hata bajaji
 
Sasa kanunua gari INA issue gani na jf ? Tuleteeni mambo yenye faida kwa watu wengi, sio hayo ambayo hayana kichwa wala miguu !
 
Ni sahihi lete mawazo ya kutujenga gari ya Wolper inatusaidiaje sisi? Vitu vingine tujiongeze wapendwa....
 
Hata Mimi nimenunua gari mbona habari yangu hamjaweka?
 
Magufuli kanunua Bomberdier mmembeza hoo Pangaboi, Lakini huyu kanunua Toyota ni Big News! [HASHTAG]#SMDH[/HASHTAG]
 
Na we we na wajinga wenzio mnaoshangaa MTU akinunua gari , forums zenu zipo, sio humu
 
Atakua ameinunua kwa hela alizopewa na ccm alipojiunga nao. Otherwise kwa kuuza ....... asingewezaununua hata bajaji
duh...ccm wameaza lini kugawa hela kwa mtu anae taka kujiunga na chama.hko mkuu?
mbna kimya kmya sna ,kama ndo hvyo kesho mapema....npate.na mimi 20ml[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] acha uwongo mkuu
 
Ni sahihi lete mawazo ya kutujenga gari ya Wolper inatusaidiaje sisi? Vitu vingine tujiongeze wapendwa....
umbea wetu tu mkuu .............gari kitu gani..ana nyumba ? mbona ujatueleza na hilo mkuu tuambie tujue
 
Renatus shughulika na mambo ya msingi, hao walionunua gari ukaamua kuitangaza wana kawaida hata wakinunua nguo za ndani zenye picha za kina" BEYONC' watakaa utupu na kujiselfie ,je Nazo utaleta jf?
 
duh...ccm wameaza lini kugawa hela kwa mtu anae taka kujiunga na chama.hko mkuu?
mbna kimya kmya sna ,kama ndo hvyo kesho mapema....npate.na mimi 20ml[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] acha uwongo mkuu
Huna taarifa eh! Tafuta kwanza umaarufu uchwara alafu ndo uende huko ili na wewe utapeliwe vizuri na lile lichama.
 
Back
Top Bottom