#COVID19 Hii hapa ni nafasi yako ya kuibadili dunia, itumie

Siyo kwamba ukipata madhara kwa chanjo basi serikali inakutelekeza.
Hapana, utasaidiwa kabisa na ndiyo maana hata ukishapata chanjo, unaendelea kufuatiliwa na unapewa namba za kuripoti pale unapopata changamoto.
Kinachozuiwa hapo ni watu wasitumie huu mwanya kujinufaisha kifedhaz uende ukafungue kesi ya kudai mabilioni ya fedha kwa kusema chanjo imekuletea madhara.
 
Sawa ila hapo sasa watakaopata madhara kweli ya chanjo wamenyimwa haki ya kushitaki.
 
Mimi mwenyewe ni darasa la saba tu mkuu ndio maana nikaomba ujapo kwa uchache uelezee hilo suala kwa lugha ya darasa la 7 japo nami nipate chochote kitu maana hiyo lugha nyengine ni mtihani kwangu.

Kwa uchache tu.
 
Mkuu,
Tabia ya kuchagua kusikia kile tu unachotaka kusikia wewe, itakukosesha mengi mazuri kwenye maisha.
usiwe mgando (fixed) dunia inakwenda kasi, mambo yanabadilika.
Kuchanja wewe ni swala la muda tu, hivyo usishupaze sana shingo, utachanja.
Sichanji.
 
"kinachoendelea ni kufuatilia ufanisi wake"

"hakuna chanjo yenye ufanisi wa 100%."
Rafiki yangu mpendwa je umeelewa ulichokiandika au umeandika tu kukamilisha mstari!!!
Inakuaje watu wafuatilie jambo lisilo na ufanisi wa 100%, je wewe unaweza kufanya kazi unayolipwa mshahara wa kukidhi mlo tu, je ukiumwa utaomba msaada kwa ndugu?
 
Mimi mwenyewe ni darasa la saba tu mkuu ndio maana nikaomba ujapo kwa uchache uelezee hilo suala kwa lugha ya darasa la 7 japo nami nipate chochote kitu maana hiyo lugha nyengine ni mtihani kwangu.

Kwa uchache tu.
Kwa uchache ni hayo niliyoeleza hapo juu, yanatosha kabisa mtu kufanya maamuzi sahihi kwenye hili.
Karibu.
 
Rafiki yangu mpendwa je umeelewa ulichokiandika au umeandika tu kukamilisha mstari!!!
Inakuaje watu wafuatilie jambo lisilo na ufanisi wa 100%, je wewe unaweza kufanya kazi unayolipwa mshahara wa kukidhi mlo tu, je ukiumwa utaomba msaada kwa ndugu?
Mkuu, kama umefanikiwa kusoma darasa nililoweka hapa, hata baada ya bidhaa kuingia sokoni, lazima iendelee kufuatiliwa.
Mfano kwenye hili la chanjo, lazima iendelee kufuatiliwa je mtu akipata kinga ya chanjo anakaa nayo kwa muda mrefu kiasi gani? Je kuna uhitaji wa kuendelea kuchoma tena ili kuboost kinga? yote hayo yanajulikana kwa tafiti zinazokuwa zinaendelea. hivyo ndivyo sayansi inavyofanya kazi na ndiyo maana tumeweza kupiga hatua kwenye maeneo mengi, kwa tafiti na kuangalia kile ambacho kinaweza kuwa improved zaidi.
 
hayo maswali yalishajibiwa, fatilia acha uvivu wa kiseng*
 
Chanjo hizi zinazotumika sasa ni zile zilizoanza fanyiwa tafiti wakati ule covid 19 inagundulika Wuhan na kwingineko duniani, tumeshuhudia wadudu hawa wakibadika na kuja kwa adhari na madhara zaidi ya yale ya awali,

Mfano Delta na sasa Lamda je bado tuamini chanjo hii ni msaada tosha ama ni sehemu ya majaribio?
 
Kwa uchache ni hayo niliyoeleza hapo juu, yanatosha kabisa mtu kufanya maamuzi sahihi kwenye hili.
Karibu.
Sawa ila huko ndio sehemu muhimu maana ndipo ambapo palifanya hizi chanjo zionekane kama zinafaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…