Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,468
- 2,349
Eti mke kwenda masomoni na mume kubaki analea watoto, ni hujuma au!
Mpenzi msomaji, lipo jambo moja ambalo nimelinasa likilalamikiwa na
baadhi ya kinababa. Linahusu wimbi la kinamama kuanzisha mchakato wa
kujiendeleza kielimu katika vyuo mbalimbali vya hapa nchini na hata
ng`ambo.
Juhudi hizo kwa upande mmoja zinaonekana ni njema, lakini kwa upande
mwingine ni aina fulani ya hujuma. Kwanini muonekano huo ulete
utatanishi? Vuta subira msomaji wangu nikumegee vionjo.
Ni kawaida katika baadhi ya familia zetu, baba kwenda masomoni na
kumuacha mkewe na watoto nyumbani.
Kadhalika hali iko hivyo kwa kinamama wanaopenda kujiendeleza
kutafuta vyuo viwe vya ndani ya nchi au hata nje kujiweka katika
ufahamu wa juu zaidi kitaaluma.
Wapo wanaolazimika kujiendeleza chini ya taratibu za kule
wanakofanyia kazi au wengine hujitegemea katika kujigharimia
kimasomo.
Swali ni je, pamoja na nia hiyo nzuri, ipo harufu yoyote ya hujuma
kwa maana ya uvunjifu wa uaminifu watu hawa wawapo masomoni?
Hivi majuzi nilikutana na kinababa fulani wakawa wanaelezea wasiwasi
kuhusu wimbi la kinamama walioolewa kuonekana wakijizatiti kwenda
kusoma na kuwaachia waume zao jukumu la malezi ya watoto.
Nilipotaka kujua kwanini kinababa hawa wanahofia mkakati huo wa
kinamama walioolewa kung`ang`ania kujiendeleza kielimu, wakawa na
haya ya kusema;
``Wengine ni janja yao tu, kwanini mama anayeishi Dar es Salaam,
aende chuo cha hapa hapa halafu asirudi nyumbani akalale huko huko?
Ukiuliza anadai eti huwa wana group discussions...kwani lazima
majadiliano yafanyike usiku? Kwanini yasifanyike mchana, halafu
akarudi nyumbani kwa mumewe? Mmoja aliuliza maswali yote hayo.
Mwingine akadakiza, ``ufisadi mtupu, mama wa Dar es Salaam kulala
chuoni na mume na wanawe wako hapa ujue ana lake jambo lazima ana
bwana wa pembeni huyu ``
Mwingine akakoleza kwa kutoa mfano, ``Yuko mke wa rafiki yangu
alipata mwanya wa kwenda kusoma ng'ambo.
Alipomaliza masomo ya miaka miwili akatarajiwa angerudi nyumbani,
lakini akazamia huko huko.
``Mume kudadisi akadokezwa kuwa mkewe alishaolewa na mzungu siku
nyingi na wala hana mpango wa kurudi nyumbani.
Kwa hiyo, mkakati wa kujiendeleza kimasomo kwa baadhi ya wanawake
walioolewa, kwa kiasi fulani umelenga hujuma na usaliti kwani wengine
wanatafutia njia ya kuondokea kama wakikuchoka``, anamalizia kusema
baba huyu.
Baba huyu wa mwisho alinikumbusha kisa kimoja ambapo ndoa fulani
ilidumu kwa miaka kadhaa bila kujibu(kupata mtoto). Wakati fulani
baba huyu akapata ajali moja mbaya ya gari.
Chanzo cha ajali ile inasemekana alikuwa akiendesha gari huku akiwa
anapapaswa na kidosho. Hamadi akajikuta anagonga kwa nyuma gari
lililokuwa mbele yake na kujiingiza mvunguni.
Baadaye akalazwa hospitalini taaban huku akiwa amevunjika sehemu
mbalimbali za mwili. Mama akachunguza chanzo cha ajali na kupata data
zote.
Alichofanya ni kumuuguza mumewe hadi akapata nafuu, kisha akatafuta
kozi yake ya nje ya nchi ambayo aliipata. Akamuacha mume huyu kwenye
wheel-chair akihudumiwa na ndugu zake, kisha yeye huyoooo akaishia
zake ulaya.
Hadi leo hii inasemekana hajarejea na huko ng`ambo tayari amempata
mzee wa kizungu ambaye anaishi naye kinyumba na wala hana mpango wa
kurudi tena huku kwani hakuacha hata mtoto. Ama kwa hakika, Maisha
Ndivyo Yalivyo. Au siyo msomaji wangu?
Kwa hili unasemaje msomaji wangu? Hebu nikupe fursa nawe uchangie
maoni tuelimishane. Hili ni tatizo linalohitaji ufumbuzi wa pamoja.
Ukiwa tayari nikandamizie kupitia;
Anti Flora Wingia
Nipashe