caven dish
Senior Member
- Sep 12, 2011
- 124
- 86
Wanajamii katika maisha ya ndoa binadamu tunakutana na mengi. Ni hili lililotokea karibuni ndio limenishangaza zaidi mwenzenu! Jamaa amemuacha mke na watoto wake na kutimkia kwa mama yake! Hii wenzangu mnaionaje?
pamoja na story kutokamilika dume zima uache familia ukimbilie kwa mama
Pamoja nakutokua na maelezo marefu wandugu swali linabaki pale pale ...hii imekaa vipi? Coz mi nimeona mkuu hapa kachemka ndio maana wanasemaje "mwanaume si maumbile tu bali mwanaume wake msimamo" na ni kitambo sasa hatua atayochukua mkewe huku nyuma atamlaumu nani?
Acha UMBEA.Wanajamii katika maisha ya ndoa binadamu tunakutana na mengi. Ni hili lililotokea karibuni ndio limenishangaza zaidi mwenzenu! Jamaa amemuacha mke na watoto wake na kutimkia kwa mama yake! Hii wenzangu mnaionaje?
Mr. ChweChwe umenifanya nikautafute umbea sasa! Asante kwa hilo nimepata mkasa mzima. Siku ya tukio jamaa alitofautiana maneno na mkewe, ndipo akakasirika na kutimkia kwa mamake na mpaka leo hajarudi na miezi kadhaa sasa imeshapita baba nanihii bado anabemendeka kwa mamake na wala hatunzi familia yake.