Hii Imepitiliza

Kiukweli hii mambo ikiendelea mambo yatakuwa si mambo. Wimbo wetu wa Tanzania ni nchi ya Amani tutausahau yani hata kwenye zilipendwa hautakuwepo.
 
Tatizo hao wagambo ni njaa kali halafu vichwa vyao ni empty. Wanashindwa kumhrumia mwanamke mwenzao hadi kuamua kumdhalilisha kiasi hicho?!
 

hoja zako ni sahihi ila zimejaa jazba mno, wakati unapaza sauti kupinga udhalilishaji paza sauti pia kuwajulisha raia wajue kufuata sheria, r u confortable kuona raia anauza chakula barabarani mtaa wa msimbazi/kongo huku pembeni kukuwa na maji machafu na rundo la taka?!. Do not just be against was the authorities does, think rationaly.
 
Dhuluma dhidi ya wanyonge itaisha lini?
Rostam azizi kwanini asikamatwe kwa mtindo huu kama kweli haki inaishi kwenye nchi hii?
 
Mh!Nchi yangu Tanganyika sijui itabadilika lini na kuaanza kuheshimu haki za msingi za wananchi!!
 
Hawa askari wa jiji wote ni std 7 failures au praimare skuli dropouts sasa unategemea nn toka kwao!
Cwapendi hawa watu... Seriously
 
jamani jamani, kazi ipo mwaka huu.....
 
Well hao ni wale wanaoitwa wamachinga wanaofanya biashara katika maeneo yasiyotakiwa. Nami pia nimejaribu kufuatilia, inasemekana huyo mama walimwambia watamkamata na yeye akawatishia kuvua nguo zote.
sasa hilo ni tatizo la mgambo au la huyo mama? maana mtoa hoja yeye anaelekeza lawama kwa mgambo tu!
 
Tatizo ni kwamba kunatatizo kubwa moja hapa africa na baadhi ya nchi za ulimwengu huu hatuliadress tumebaki tukilaumu ccm pekee nalo ni unemployment kwa vijana. Hakuana mikakati ya dhati ya kuwafanya vijana ambao kwa sasa ni special group kutafuta ajira binafsi, serikali, mashirika binafsi na NGOs kutafuta namna ya kutafuta ajira mbadala kwa vijana. Nakumbuka Mwalim Nyerere kwa kutambua hilo aalianzisha viwanda vingi nchini na kilimo cha ujamaa lakini kwa ubinafsi wa mapuppet waviua ili wazungu na waasia wapate soko. Ushauri wangu kwa wana JF tusaidiane mawazo hata kama ni kuishinikiza serikali ya CCM ing'oke na iingie ya chama kingine, kuwe na hoja nzito ma yenye manufaa kwa wa TZ
 
hii ni dalili kuwa watu wamechoka na wafanya wawezalo kutambua haki zao... ndo maana wako tayari kuzipigania... tartiiibu....tutafika tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…