hii imetokea dodoma

kiapo kipo sawa, tuache kuweka fikra za udini mbele, itafikia watu hawataweka status ya Dini kwenye cv zao eti wakihofia watabaguliwa makazini. Swala la msingi ni wahitimu gani tutawajenga udom huku wakiwa wamejengewa hofu kiasi hiki? Naamini kuthubutu na kusimamia haki zako ni part n parcel ya elimu. Nadhani wanafunzi badala ya kudai haki zao hadharani watadai kwa siri kwani mnaweza kuamka chuo kimechomwa moto.
 
ninachokiona hapa ni vitisho/ubabe haya wadogo zangu akufukuzae hakwambii toka, mvumilie tu mmalize chuo hayo mambo mengine ya kudai haki yawekeni pembeni kwa muda uliobaki maana hicho kiapo wakiamua kuwa serious hasara itakuwa kwenu, well sijui kama sasa hivi tz kuna credit transfer
 

NAHISI ENZI ZA MANAMBA INA ZINAREJEA NCHINI. Wanasheria mko wapi? Tunaomba mtufafanulie sheria ya kiapo inatumika maeneo yapi? Hii ya chuoni nimeiona UDOM. ikifanikiwa hapa itatumika sekondari, shule za msingi na hata tutakapoingia ofisi za serikali kupata huduma.
 
Kuonyesha imani ya dini kwenye kiapo hicho ni makosa. Affidavit za kuthibitisha uraia au kuzaliwa mbona hazina mambo ya dini na mimi ninazo affidavit zilizosainiwa mahakamani, na hakuna mahali popote suala la dini limeonyeshwa. Nadhani kuna kitu kimekusudiwa.
 

FaizaFoxy, hivi ni viapo fake hakuna kitabu chochote cha dini wanchoshikishwa hawa vijana wala sidhani kama kuna hakimu au wakili anayesimamia hivyo viapo labda wanasheria watatujuza zaidi
 
nashangaa kiapo sijui ndo mwisho wakudai haki zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…