hii ina ''apply'' kwa mahakimu tu au na fani nyingine?

hii ina ''apply'' kwa mahakimu tu au na fani nyingine?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
nafahamu hakimu anaweza kujitoa kusikiliza kesi yoyote mfano pale anapokuwa na maslahi na hiyo kesi. je wafanyakazi wa fani nyingine wana hiyo nafasi? mfano, askari anaweza kukataa kumkamata mtu anayetenda kosa la jinai kwa kigezo hiko cha mgongano wa maslahi, kama vile kumkamata baba yake mzazi au ndugu mwingine wa karibu aliyetenda kosa yeye akishuhudia? au daktari yuko kazini, kisha analetwa jambazi aliyejeruhiwa vibaya kutibiwa, kabla hajamtibu anagundua kuwa jambazi huyu aliwahi kuvamia nyumbani kwake kufanya uporaji ambao pia ulihusisha mauaji ya mwanafamilia yake, je anaweza kukataa kumtibu (hapo yeye ndiye daktari pekee mwenye ujuzi) bila kuhatarisha kazi yake? maana anaweza kumtibu kwa kinyongo yule jambazi akafa kama akilazimishwa? je huu mgongano wa maslahi unaruhusiwa kwenye fani zipi?
 
mmmhhh hapo shughuli ipo ungeipeleka sheria ingefaa kweli..
 
Back
Top Bottom