Naona jinsi gani watu wetu wengi hasa vijijini bado ni WADANGANYIKA.
Waache waende leo sokoni kupata punguzo la bei ya bidhaa halafu watoto wao zendelee kukalia mavumbi, watembee uchi ama wawe wanavaa fulana za CCM na wamama wajawazito waendelee kulala mzungu wa nne.
Ooh nimesahau, waendeelee kulala gizani kwakuwa umeme haupo (thanks kwa wajasiria malio wanaoleta umeme jua siku hizi, japo matanga mnayapunguza) na wendelee kubaki na MAHANDAKI wanayodanganywa kuwa eti yanaitwa "BARABARA"
Mimi siupendi unafiki na ushabiki usio na mantiki, lakini MNAFIKI NA SHABIKI ASIYEJUA ASHABIKIALO huyo simpendi KABISA