Hii interview imenishangaza

Dah. Kama sikosei ni among the Big 4 Auditing firms ndio wana utaratibu huo.omba Mungu upate kazi hiyo,wako serious sana hao.achana na upuuzi wa huko utumishi ulikozoea.
 
Dogo umenikimbusha mwezi Julai nipokuwa member wa panels ya NGO fulani ya kigeni kuwafanyia interview waajiriwa wapya. Wasailiwa wengi walikuwa wanatetemeka kuona wazungu. Na Mara nyingi walikuwa walishindwa kuelewa maswali na kubaki kusema,....cammon' again!? (Come on again)

Nilichogundua baadhi ya wasomi wetu wana skills nzuri kwenye kuandika lakini kwenye kusikiliza na kuongea kuna shida. Hasa wakiwa wanafanyiwa interview na wazungu wanashindwa kabisa kujiamini hasa wale ambao hawakuwahi kabisa kukutana na kuongea ana kwa ana kabla na ngozi nyeupe.
 
Wewe ni mshamba kama ulivyosema, bado unaishi enzi za ujima na haupo tayari kuishi kwenye zama ambazo technology imeendelea...mm binafsi katika interviews nilizofanya hamna ambayo ilikuw chini ya 30 mns na my last interview ya sehemu niliyopo saiv ilifanyika kwa saa 1...nakushangaa wewe dakika 15 unaona nyingi
 
kilaza huyu na hapo ana degree gpa 4.5, yaani vyuo vyetu haviwapi kabisa hawa vijana exposure
Ni huyu akiajiriwa serikalini ubunifu zero hajui hata Microsoft teams hata problem solving ni zero kazini. Mitaala ifundishe wanafunzi ubunifu pia kuendana na nyakati za sikuhizi
 
Ila hizi interview hizi, some years back nikiwa huko Mtwara maisha yamekaba kila idara, jamaa yangu akanitumia job advert from NGO moja inahitaji watu kwa fani mbalimbali. Nikaona one of the vacancy posts ni eneo langu la kujidai, faster nikatengeneza CV ili iendane na hitaji lao,then nikawatumia pamoja na cover letter. Yaani the same day jamaa waka acknowledge kupokea maombi yangu na kuambiwa nikipita mchujo nitaitwa na kama sitaitwa ndo nijue sikubahatika. Basi bwana nikakaa miezi miwani ikapita nikajua ndo ntolee hiyo nimekosa but ghafla nikapigiwa simu na kuambiwa nicheki email kwani natakiwa kwa interview. Kucheki email kumbe kweli bwana imetumwa two days ago nami nilikuwa sijacheki. Nikatafuta nauli nikafunga safari to Dar, nikafika wakanielekeza nikafika kwenye ofisi yao. Baada ya nusu saa nitaitwa kwenye ukbumbi kuna watu 5 wazungu 2 wengine wabongo wenzetu, aisee walinikaanga kwa maswali for more than two hours. Mwisho wakanishukuru na kuniambia niingie chumba kingine, nikapelekwa kwenye computer nikapewa karatasi yenye maswali ya kujadili issues mbalimbali kama conflicts management, funds management etc kwa muda wa robo saa nikimaliza niisevu hiyo kazi kwa format fulani na jina fulani and then niitume kwenda email niliyopewa pale. Nikakomaa nikamaliza na kuipa jina, nikaisevu na kutuma. Baada ya kumaliza yote nikapelekwa idara ya fedha nikaambiwa jazi hii fomu aisee sikuamini wale jamaa wakanilipa night allowance mbili za Dar kwa rate ya 100,000 enzi hizo per night. Pia nikaulizwa una tiketi ya Bus, nikachomoa tiketi nikawapa wakanirudishia nauli ya kuja na kurudi, yaani sikuamini kabisa!!
 
Usiniite mshamba.kwani wewe unajua kila kitu hapa duniani?
Ulikuwa mtu mshamba maana hujawahi kufanya interview za hizo so kuwa mgeni wa jambo ndio ushamba wenyewe, hata mimi na ushamba wangu kwa mambo mengine pia nisiyo yajua
 
Kwamba mnaamini jamaa hajui? Ni amekuja kutuoshea kwamba siku kadhaa mbele mshahara utaanza kusoma 7M kwa mwezi na hapa anaangalia nani atamtukana ili awe anamuoshea zaidi akishapangiwa eneo la kazi.
 
To cut the story short bro... Huo mchongo umeupata au wamekupiga chini?
 
Watanzania bhana wakenya wakiwabeza mnasema wanadharau but sio hivyo
Ukweli ni kwamba tuna kizazi Cha ajabu sana
Tunaposema Tanzania hakuna elimu mnakataa ila ndio ukweli
Ila pole Kaka ushapoteza kama Yanga juzi[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Spika zilikuwa sawa, shida ya waswahili wengi listening skills ni tatizo
 
Ningekuwa na connections na vyuo ningekuwa nawapiga msasa lwenye elimu na uhalisia. Shida wamejifungia huko wakija huku wanakutana na shule mpya ya mtaani
 
Ulikuwa mtu mshamba maana hujawahi kufanya interview za hizo so kuwa mgeni wa jambo ndio ushamba wenyewe, hata mimi na ushamba wangu kwa mambo mengine pia nisiyo yajua
Mjuaji wa kila kitu wewe humu jf.
Sawa umeshinda boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…