[h=2]NSSF kuokoa fedha za kigeni kwa kujenga kliniki za magonjwa makubwa nchini[/h]
Na Mwinyi Sadallah
2nd December 2012
B-pepe
Chapa
Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeanza kutekeleza mradi wa kutibu magonjwa makubwa utakaofanyika nchini badala ya kuwapeleka wagonjwa ngambo, hatua itakayopunguza matumizi ya fedha za kigeni kwenye tiba.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk.Ramadhan Dau, alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa kliniki tano za kisasa zitakazotoa tiba kwa njia ya video na mtandao.
Akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri unaofanyika mjini hapa Dk.Dau alisema mradi huo unatarajia kukamilika Febuari mwakani na kituo kikubwa cha tiba na uchunguzi kitakuwa jijini Dar es Salaam.
Dk.Dau alisema NSSF imeingia mkataba na hospitali ya Apollo ya India na madaktari bingwa wa hospitali hiyo watatoa tiba kwa mtandao ambapo mgonjwa atakuwa Tanzania na vipimo vyake vinachunguzwa na wataalamu wa India na kurudisha majibu ili kuanza kutoa matibabu.
"Madhumuni ya hizi kliniki ni kupunguza gharama za matibabu watu kwenda India kitakachofanyika ni kwamba mtu kama anaumwa atakwenda kwenye kliniki atafanyiwa vipimo vyote, ambavyo angeweza kufanyiwa India na katika makubaliano yetu watu wa Apolo wamekubali mashine zote zinazohitaji kufanya vipimo wataleta wao" alisema Dk.Dau.
Alisema mradi huo utainufaisha pia Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo itajengwa kliniki itakayotoa tiba kwa kutumia teknolojia hiyo ya uchunguzi wa magonjwa makubwa ambapo wagonjwa watakuwa Zanzibar lakini watachunguzwa India.
Alitaja mikoa mengine itakayonufaika na mradi huo kuwa ni Mwanza, Arusha na Mbeya, ambapo Sh. bilioni 4.8 zitatumika na kuelezea kuwa hatua itakayofuata ni ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa ya Apollo na kwamba mradi huo upo katika hatua ya michoro.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula, alisema mradi huo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi na utawanufaisha hata wasio wanachama wa mfuko huo.
Alisema lengo kubwa la NSSF ni kupunguza gharama za matibabu iliyokuwa ikipata serikali kwa kuwatibu wananchi na viongozi, kuboresha huduma za afya na kuwajengea uwezo madaktari kwa kutumia teknolojia mpya za kisasa za tiba na uchunguzi.
Aliongeza kuwa NSSF imesaini mkataba na hospitali ya Apolo, mwaka jana na kushuhudiwa na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh na kuongeza kuwa kliniki kubwa mradi umeanza katika makutano ya Barabara za Bibi Titi na Morogoro.