Hii itasisimua kuliko ya Kaseke

Inawezekana kabisa kwa yanga. Ila nina wasiwasi kama kweli ni maelekezo ya pluijm kwani yeye naye anakuja na mawinga 2 waghana + ngoma wa platnum. Yanga wasipokuwa waangalifu yatawakuta yaliyowakuta simba msimu uliopita kuvunja mikataba na wachezaji kabla ya ligi haijaanza matokeo yake kulipa pesa nyingi na kuacha wachezaji wazuri na kusajili wachezaji walioshindwa kuonyesha uwezo wao.
 
mvuv huyu ni nani?
 
Last edited by a moderator:
Nijuavyo mimi wachezaji huwa wanabadilishana jezi baada ya mechi na huwa wanazitunza kwa kumbukumbu au kuzivaa wakati usio rasmi. Kipre alijua akiivaa hapa bongo italeta mkanganyiko, so ameenda kuivalia huko huko Abidjan

 
Wachezaji ambao walivuma katika vilabu vyao kisha Yanga ikawasajili kwa mbwembwe za 'kuipiga bao Simba':

Hussein Javu - ameachwa
Said Bahanuzi - ameachwa
Dan Mrwanda - ameachwa
Hassan Dilunga - anatolewa mkopo
Shaban Kondo - ameachwa

Simba imekuwa ikiichezea akili Yanga kwa kujidai inamtaka mchezaji fulani, Yanga nayo inatoka nduki na milioni zao 40 plus mshahara wa milioni mbili, na kumsainisha haraka haraka kisha kupiga naye picha na kusema 'imeipiga bao Simba'. Kwa ufupi Yanga ina hela 'za kuchezea' ndio maana kutoa milioni 40 kwao ni rahisi tu. Ila nina wasiwasi mfadhili akikata mrija sijui hiyo mishahara minono itatoka wapi!
 
Hiyo ya kuchezewa akili na watani kama ina kaukweli fulani maana nikiaangalia haraka haraka usajili ambao umeshafanyika jangwani mpaka sasa hivi haihitaji kuwa mtaalamu sana wa mpira kuona tatizo. Au ndio maana wamekimbila tff kuomba wachezaji wa kigeni waongezwe wafike 8.
 
Wangekuwa wanaichezea Yanga halaf wanashika hata nafac ya pili wange tushtua lakini kama wana ichezea halaf wakijitahid sana nafas ya tatu huku yanga wakichukua ubingwa nadhani kwa hali hii ni unaweka mtego halaf mtego unakunasa mwenyewe mtegaji na ndo maana Rage aliwaita lile jina.......
 
 

Tunajua sasahivi simba iko gonjwa gonjwa hakuna pesa ya kusajili wachezaji wa kiwango cha kimataifa. Kuweni wapole tu kwanza Yanga tukimaliza usajili nanyi mtaweza kusajili wale tuliowaachia.

Hakuna cha friends of simba wala nini hadi Ramadhani Singano anawatoa jasho kwakuwa mmefoji mkataba wake na kuuongezea mwaka mmoja ili uwe wa miaka mitatu wakati mlisainishana mkataba wa miaka miwili tu.
 

Mbona unawataja nusu nusu Umewasahau
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
 

huko kuchezewa akili na mtani kumeifanya simba kufanya kipi cha maana katika soka la hapa bongo? Mbona sasa ni msimu wa tatu tunaelekea wa nne no ubingwa no nafasi ya pili no mashindano ya caf mmebaki kukodoa macho kwenye kideo tu...wako wapi wa akina daniel akufo Dan serukuma simon serukuma, na wengine mnaowajua wenyewe,,,
 

Dan & Simon Serunkuma wapo Uganda na Daniel Akufo yupo Malaysia.
 
Makendaa una akili sana wewe.
 
Last edited by a moderator:

we jamaa jibu lako limejitosheleza halihitaji nyongeza bila shaka mambumbumbu wamekusoma vizuri kabisa
 
Mbona unawataja nusu nusu Umewasahau
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
Hivi huna taarifa kwamba Plujim amependekeza Yondani aachwe? Sijamtaja kwa kuwa bado viongozi wanavutana. Mbuyu Twite naye ameambiwa amezeeka, amepewa mwaka mmoja kwa hela ya usajili ambayo hata wachezaji wa ndani wanaikataa!
 
Simba inamuhitaji Themi Felix; heee, Yanga watakavyotoka nduki kwenda kumsainisha haraka haraka! Na picha juu na kukabidhiwa jezi, kisha mwakani inamtoa mkopo!
 
Tunajua sasahivi simba iko gonjwa gonjwa hakuna pesa ya kusajili wachezaji wa kiwango cha kimataifa. ..
Hivi wachezaji ambao timu yao ikijitahidi sana inaishia raundi ya kwanza, nao ni wa kimataifa? Kucheza Comoro na Botswana nako ni kuwa kimataifa?
 
Hivi wachezaji ambao timu yao ikijitahidi sana inaishia raundi ya kwanza, nao ni wa kimataifa? Kucheza Comoro na Botswana nako ni kuwa kimataifa?

Sasa iko timu ambayo hata nafasi ya kuingia raundi ya kwanza haipati. Yenyewe inasajili kwa ajili ya mabonanza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…