Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,051
- 461
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova
Polisi kwa kushirikiana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, wameanzisha mchakato wenye lengo la kuyafanya maduka yaliyopo Kariakoo yafanye kazi hadi saa sita usiku.
Kwa mujibu wa utaratibu uliopo sasa, maduka hayo yanafungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, jeshi hilo linawasiliana na wafanya biashara wa eneo hilo, ili kuanza majadiliano.
Alisema hatua ya maduka hayo kufunguliwa hadi saa sita usiku itasaidia kuongeza kipato cha wafanyabiashara, kukuza uchumi na kupunguza msongamano wa watu.
Kwa mujibu wa Kova, masuala ya msingi yatakayopewa kipaumbe katika mchakato huo ni yanayohusu ulinzi na usalama.
Kova alisema majadiliano hayo yamelenga kuimarisha ulinzi wa kutosha katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu ya kuweka taa kubwa na kufunga kamera za kuwabaini wahalifu.
Pia alisema mchakato huo utajumuisha kuanzishwa njia za simu ambazo zitatumika kwa haraka katika kutoa taarifa za uhalifu.
"Hatua hii itawasaidia hata watu wanaotoka kazini jioni, kwenda madukani kununua bidhaa pasipo uharaka wala msongamano, alisema.
Alisema jambo la muhimu kwa wafanyabiashara hao ni kuzingatia masharti yanayohusu ulinzi.
Wakati huo huo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 11 wanaosadikiwa kuwa majambazi sugu, wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali jijini hapa.
Miongoni mwa makosa hayo ni ujambazi wa kutumia silaha, wizi wa televisheni, pikipiki za miguu mitatu bhangi na gongo.
Kova alisema kuwa bado wanaendelea na operesheni ya kuwasaka majambazi sugu kwa lengo la kuondoa uhalifu jijini humo...
UCHUKUO WANGU..
Ujambazi unakua kwa kasi ya ajabu tz hata mchana je wakianzisha hii maduka mpaka usiku kutakalika kweli Kariakoo jamani?KOVA ATAWEZA KWA HILI