Wakuu, maneno huumba. Hivi karibuni pana hii kauli mbiu ya kuufanya mchezo wa soka ni vita.
Soka ni soka tu na vita ni vita tu sasa hawa wanaotupeleka kwenye vita badala ya soka wana lao jambo.
Nchi zilizopigana vita raia wao hawataki kulisikia neno hili, Sisi tunalitumia kama njugu.
Nimesoma kuwa msemaji wa serikali kakemea maafisa wa habari kusema porojo badala ya kufuata taaluma ya habari. Wito wangu na hili alikemee pia.