Hii kesi yangu ikoje au ndo kua mara yangu kwenda mahakamani

Hii kesi yangu ikoje au ndo kua mara yangu kwenda mahakamani

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Mnisaidie nitafungwa

Nlikamatwa hapa kwetu kulitokea taharuki vurugu watu wakafanya vurugu kituo cha polisi kuvunja kwa mawe na kuchoma gari la raia aliekua amepaki maeneo ya kituo, Baada ya kuja wale wakutuliza vurugu zile mimi walinikuta nikiwa nafunga duka wakanichukua na kupelekea duka kuliacha wazi

Tulikamatwa watu 100+ tukapelekwa mahakamani tulisomewa mashitaka kwapamoja hatukupata nafasi yakueleza jinsi tulivyokamatwa, tulikana kwa pamoja tukapelekwa mahabusu badae tukapata mdhamana tukatoka tuhudhuria kuskiliza kesi yetu,

sasa mimi wasiwasi wangu leo hii ni awam ya pili mahakamani tukifika ni kuhesabiwa tu na kuambiwa tutarudi tarehe nyingine hatupati nafasi ya kujieleza mmoja mmoja jinsi alivyokamatwa, mfano mimi nilikutwa eneo langu la kazi nikijiandaa kufunga kufuri za duka niende nyumbani.
 
Unaweza filisiwa waona....Mungu akusaidie
 
Kesi ya kufungwa zip mbili kuua na kubaka hizo zingine ni simple as possible
 
Una hela? Kama una hela waone wahusika ( polisi au waendesha hayo mashitaka).
Utajikuta tu mahakamani huudhulii na kuacha watu wakijiuliza mbona mwenzetu haendi?
 
Relax case za hivi huwa ni ngumu kwa upande wa serikali kushinda .
 
Kesi za hv huwa za kijinga sana,kuna kijiji kiliua mtu toka 2017 mpaka leo kuna wengine bado wameshikiliwa na kuna ambao walikamatwa walikuwa wanapita tu hapo kijijin hata sio wakaz wa hapo
 
Kesi za hv huwa za kijinga sana,kuna kijiji kiliua mtu toka 2017 mpaka leo kuna wengine bado wameshikiliwa na kuna ambao walikamatwa walikuwa wanapita tu hapo kijijin hata sio wakaz wa hapo
Hata hii ina watu walikamatwa stendi wakiwa wamesubiri usafiri
 
Kesi haijaanza kusikilizwa hiyo, ikianza kusikilizwa watasikilizwa Jamhuri baadae na nyie mtapewa nafasi ya kusikilizwa utetezi wenu. Kwa hiyo usijali wakati ukifika utatoa maelezo yako.
 
Back
Top Bottom