Hii Kozi Ya Multimedia and Film Production, Zipi Fursa zake?

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
6,260
Reaction score
14,470
Ndugu wana JF naomba Kuuliza,

Hii kozi ya Multimedia and Film Production, inayotolewa pale DIT.
Ikoje haswa, na ni zipi fursa zake kwenye kujiajiri na hata kuajiriwa.

Nimeona kwenye prospectus ya DIT wanatoa kuanzia level ya Basic technician hadi diploma huko.

Vipi kuna chuo kingine hapa tanzania wanatoa hii kozi.

Nina mdogo wangu kamaliza darasa la 12, nataka apite huko.

Asanteni.
 
Sasa si uende DIT ukapate ufahamu vizuri.
 
Awa wajinga walio reply hapa hawaelewi kuhusu multimedia.
Hiyo ni course yenye mchanganyiko wa visual, graphics na makolokolo yote ya media.
Atajifunza kutengeneza videos, kudesign graphics, basics za softwares mbalimbali.
Ajira au kujiajiri ni video producer, kutengeneza mabango, posters, cards, IDs, smartcards, audio production kama nyimbo, matangazo, podcasts, vipindi vya radio tv. Mitlimedia ina mambo mengi sana.
Achana na awa wachawi walioreply hapa hawajui lolote kazi yao ni kukunja tu.
 
Mkuu kwenye kuchagua kozi ya Kusoma kuna mambo mengi sana ya kuangalia.Je Mdogo wako Mpaka anamaliza Darasa la 12 ana interest na hayo Mambo ya Multimedia and Film Production?Kama Jibu ni Ndio Basi Fursa zipo Nyingi sana kwani Hii Kozi inahusisha TIKTOK,YOUTUBE,ADOBE,RADIO,MUSIC/UDJ,Graphic Design.n.k.

Je Hayo ni maeneo ambayo anayapenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…