Hii Ligi Kuu ya Ulaya ni utata mtupu

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Chama cha vilabu vya soka barani Ulaya, ECA, amabcho kinawakilisha vilabu 246 Ulaya yote, kimeandika barua kwa Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA, kupinga mpango wa baadhi ya vilabu kuanzisha ligi yao, Ligi Kuu ya Ulaya.

Cha kushangaza ni kwamba, Rais wa Chama hicho ni Andrea Agnelli, ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Juventus ya Italia ambayo ni moja ya vilabu vilivyosaini kuanzishwa kwa ligi hii.

Mbaya zaidi, Agnelli ni rafiki wa karibu wa Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin, ambaye anaupinga sana mpango huu.

Ina maana Agnelli amemsaliti rafiki yake, Rais wa UEFA, lakini pia ni kama chama anachokiongoza pia amekisaliti.

LIGI YENYEWE

Ligi hii ni wazo la tangu miaka ya 1980 lakini kwa sasa liliibuliwa upya mwaka 2009 na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez pamoja na matajiri wa kimarekani wanaomiliki baadhi ya vilabu vikubwa vitatu vya England; Manchester United, Liverpool na Arsenal.

Benki kubwa ya Marekani ya JP Morgan itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano haya yatakayoshirikisha timu 20, lakini 15 kati ya hizo zitakuwa za kudumu kwa miaka 20 huku 5 zilizobaki zitakuwa zikipanda na kushuka daraja.

Perez anatarajiwa kuwa Rais wa ligi hii, huku wamiliki wa Liverpool, John W. Henry, wa Manchester United, Joel Glazer na wa Arsenal Stan Kroenke, wakiwa makamu wa Rais kwa pamoja.

Mwenyekiti wa Juventus, Andrea Agnelli, atakuwa makamu wa nne wa Rais, nyuma ya wale makamu wa watatu.

Muundo wa ligi hii ni sawa na ule ambao Rais wa FIFA, Gianni Infantino anataka kuleta Afrika.

Kama Ulaya hawaitaki, sisi nani tuukubali?
 
Kazi inaendelea
 

Attachments

  • michaelnguli_1618847501202.jpg
    151.4 KB · Views: 2
Uzuri halitafanikiwa, likifanikiwa ndo mwisho wa EPL
 
Wanataka kuharibu mpira hawa. Kuna timu zimegundua hazina uwezo wa kuchukua uefa maisha yao yote sasa wanataka kujaribu bahati yao kwa kuharibu mashindano bora kabisa. Inakuwaje timu 15 ziwe lazima kushiriki ht bila kutoa jasho kisha waseme ni mashindano hapo hakuna mashindano
 
Tunakoelekea iwepo world supercup/leagues kila bara litoe timu nzuri zikashindane Tz simba ipo [emoji23][emoji23][emoji23] ...

Ngoja tusubirie ya Africa kwanza
 
Tunakoelekea iwepo world supercup/leagues kila bara litoe timu nzuri zikashindane Tz simba ipo [emoji23][emoji23][emoji23] ...

Ngoja tusubirie ya Africa kwanza
Hii mbona ipo na kwa sasa bingwa ni bayern
 
Kwa africa itatusaidia ila sijui tu itatusaidiaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…