Judgement
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 10,326
- 4,785
Ilikua ni siku ya Jumamosi tupo harusini na muda husika niuzungumzao ni tulipokua ukumbini, harusi ambayo mmoja ya mdau mwenzangu kazini alikua anaoa.
Mimi na mama ya boma yangu (wife) ni miongoni mwa wageni waalikwa, shughuli iliendeshwa vizuri kwa mujibu wa ratiba ilivyoainisha tulikunywa tukala kama ilivyo ada.
Ukafika wakati wa muziki mimi nilim'nyanyua wife nikacheza nae takriban nyimbo mbili, wife alikua akicheza kwa style zake za kawaida kama nilivyozizoea sikuona kipya tukarudi kukaa vitini kuendelea na vinywaji huku tukiwaangalia waalikwa wenzetu wakiendelea na miserebuko, ghafla akatutokea mdau mwenzangu wa kazini ambae na wf wangu anam'fahamu (kwa taarifa huyu kijana yeye bado hajaoa) japo kwa marika mimi na yeye hatupishani sana.
Huyu mdau akaniomba akacheze na shemejie, na kwa dunia ya leo ya (global, dotcom,twiter e.c.t) si rahisi kulikataa suala kama hilo! Nikam'ruhusu wakachezenae, ambapo eneo walilokua wakicheze ni mbele ya meza tuliokua tumekaa nilichokishuhudia hapo sikuamini macho yangu vizuri ni kwamba wife wangu alikua anakata MAUNO ya nguvu! MAUNO ya ukweli ! MAUNO ambayo sijapatapo kuyaona hapo kabla, MAUNO! alikua anakatika kama umuanavyo "funza wa chooni" au kuzidi! tangu nimuoe sikuwahi kujua kama mama ya boma ni mkali wa kucheza kivile. Sio siri kisukari changu kilipanda ghafla nikijiuliza kama wife wangu ni mkatikaji kivile mbona hata siku 1 hajawahi kunikatia mie mumewe? Na iweje mikatiko ile akakatikiwe mdau ? Mdau ambae hata kuoa hajaoa? Hata wife anaelewa hivyo? Aidha iwe ameoa au bado still sioni reason yeyote ile mdau au nje ya mdau atakaekua na right ya kuchezewa MIUNO ile tofauti ya mie MUEKEZAJI !
Nilitamani nikawakatize kabla nyimbo ile haijaisha lakini namshukuru Mungu nilifanikiwa kulidhibiti hilo, na wimbo ule ulipokwisha sikuhitaji tena kuendelea kuwepo ukumbini pale, nilimwambia tuondoke kidogo akataka kuleta ubishi na aliponiona sitanii naelekea kutoka huku nikimuacha akanifata, njia nzima tukiwa garini ni ukimya ndiyo ulitawala.
Tulipofika home ndipo nikaiweka agenda mezani nikitaka maelezo toshelevu dhidi ya kadhia nzima ya kile kisicho cha kawaida nilichokiona ukumbini (MAUNO YA HATARI KWA MDAU) Jibu alilonipa namnukuu "Wewe ndiyo hua hunichezeshi kuendana na bit za nyimbo! Hua unacheza slow-slow namie ndiyo inabidi niende slow! Yule jamaa yako alikua ananichezesha kwa kasi ya bit ya nyimbo na ndiyo maana namie nikawa naenda kasi"
Wadau je? Hizo ni sababu toshelevu kweli kwa wife wangu kumuonesha maufundi na maujuzi ya MAUNO shemeji yake? Hapa kweli mtaniambia mambo ya "inferiority cmplx?" sijanyanyaswa/sijadhalilishwa hapa? Au kuna "behind the curtain" between mdau with my wf?