Hii nayo inahitaji ujuzi zaidi

Hii nayo inahitaji ujuzi zaidi

Nicodemas Tambo Mwikozi

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2016
Posts
663
Reaction score
1,047
Ninasoma saana humu ila mwezenu napenda kula local food

Mfano chai nasindikiza na maboga mamung'unya mahindi ya kuchemsha viazi Karanga nk

Kwa kawaida hivi hua vinahitaji maji tuu chumvi mzigo unaamka

Swali je kuna mtaalamu humu ambaye ana ujuzi mpyaa wa kutengeneza hivi vitu vema zaidi...

1474847583264.jpg
1474847635619.jpg
 
Wasukuma bhana wanatabu kweli kweli.


Kuna vyakula havichanganywi hovyo hovyo.

Mahindi na maboga!!!!!!
Hiyoo garama ya mahindi punguza uwe unanunua robo kikombe ya maziwa chai.
 
Kula nako ni mpangilio. Hayo mahindi yote na maboga labda kama mko watu kadhaa. Ila naona kikombe kimoja!

Hayo maboga yote unapata vitamini A nyingi sana kuliko unavyohitaji kwa siku na kama unafanya hivyo mara kwa mara kuna hatari ukawa na mifupa teketeke ukiguswa tu ugoko mpirani unavunjika hovyo.

Hayo mahindi umekula wanga mwingi sana kwa asubuhi. Labda kama unafanya kazi za mitulinga siku nzima. Hindi moja lingetosha kwa kazi za kawaida. Wanga wa asili km hivyo ni mzuri unapata na makapi.

Kuhusu kupika huna haja kutumia chumvi nyingi. Weka kdg sn au badala ya chumvi waeza tumia malimao na tangawizi kunogesha.

Kuboresha msosi wako wa asubuhi weka hapo yai 1 la kuchemsha au vipisi 2 vya nyama saizi ya kidole chako gumba.

Weka pia mbogamboga ambazo zenyewe waeza unga na mafuta kdg labda kijiko cha chai maana nayo muhimu asubuhi (ingekua unakula mkate basi ungetumia siagi). Ila zisiive sana. Kaanga kitunguu kilete ukahawia wa mbali tia humo karoti kdg bamia zilizokatwakatwa na gilgilan. Tia mbogamboga zipate tu moto kuuwa wadudu kisha ipua pakua tenga kula.

Ongezea karanga au korosho au jamii za mikunde au maharage ili upate protini za mimea. Zinafaa sana kuendena na protini za wanyama kwa 7bu tu za kilishe. Waeza zichemsha na hayo mahindi lakini uyaondoe kwenye gunzi kisha changanya na maharage au karanga kwenye sufuria moja.

Shushia na mtindi nusu glasi usio na sukari. Labda asali nusu kijiko cha chai. Kama wapenda chai basi ya maziwa fresh na ni km huna aleji nayo (hili la maziwa nalo somo pana la lishe na utabibu)!

Vyakula vyote hapo juu ni kifungua kinywa na havizidi sahani moja. Kipimo cha hiyo sahani kwa wastani kiwe mikono yako miwili ikiwekwa kama vile unakinga maji unywee bombani.

Vyakula vya asili ni vizuri sana km una uwezo kupata na una muonjo navyo.

Tahadhari. USIVIIVISHE SANA upikapo isipokua nyama!!
 
Hilo pumpkin limekua baked?

Nna shosti wangu mpishi mzuri kila nkienda kwake akinikaribisha kula huwa namdai dessert ndivo tumezoeshana siku kanikomesha Na boga la ku bake lol
 
Dar wanaboresha mahindi ya kuchoma kwa kupaka chumvi na pilipili....
 
Back
Top Bottom