Hii nayo kero

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
8,597
Reaction score
1,690
Salaaamu wakulu!
Yaani mke kaingiwa na imani ya dini ajabu! Basi kila siku 1 ya juma anaenda kushinda kwenye mkesha kanisani! Tena unakuta ni mwisho wa juma ambapo unamuhitaji sana hasa kwa mapumziko! Na kesho yaki akirudi atalala kutwa nzima kisa amekesha! Mzee unajichukulia time unaenda kupiga mitungi na ukirudi balaa jingine " lecture" zinaanza duh yaani tabu kweli kweli! Hapa msaada gani unafaa .............hehe hiki ni kikomo cha magari mabovu tena duh.
 
Najaribu kufikiria kama nimuweke huyo mwanamke kwenye lile kundi ila bado sijapata jibu nafanya:confused2:
 
shukuru Mungu ameokoka maana angeamua kuwa sister du ungemfukuza
 
Nilikuwa sikubaliani nao na sitakubaliana nao, lakini katika hili sina budi kumshauri mume ajiunge 'infidelity'.
nawajua jamaa ambao wake zao wanadai wanashinda kanisani lakini mara nyingi huwa nakumbana nao kwenye kumbi za starehe na wanakesha, sina maana na huyu ni mmoja wao, lakini kwa kukidhi haja ya moyo si mbaya nae mwanaume akiongeza maombi na akijiunga infidelity kujipoza kidogo.

NOTE: UKIMWI upo na unaua
 

Hapo maamuzi ni magumu:confused2::confused2::confused2:
 
How sure are you? Anapoenda kwenye mkesha are sure anaenda kwenye mkesha kweli?

Kumbe una wasiwasi? real pole ila kwa mwanamke mwenye busara bado atakua na muda na mumewe kaa chini uongee nae
 
Kumbe una wasiwasi? real pole ila kwa mwanamke mwenye busara bado atakua na muda na mumewe kaa chini uongee nae

Wakasome kitabu cha " WIMBO ULIO BORA" :confused2:
 
ni suala la kukaa nae chini mkaongea

mueleze kwa upole lakini hakikisha huyumbishwi katika kuwasilisha hoja yako.

mueleze kuwa yeye ndio sababu inakufanya ukalewe nje na itakupelekea kuingia kwenye club ya infidelity bure.
 
Kumbe una wasiwasi? real pole ila kwa mwanamke mwenye busara bado atakua na muda na mumewe kaa chini uongee nae

Siri anayo mwenyewe kama kweli anaenda au anaenda kwenye mambo yake still kwenda kwenye mkesha si chanzo cha kusema ameokoka kwani hauwezi kukesha nyumbani kwako unasali
 

Nilikuwa sina wasiwasi na wewe kwa kuwa najua bado uko kwenye chama
 
Labda jaribu siku moja kuunga tela mkakeshe pamoja! Baada ya hapo, sema nae tu.

Yaani unanihakikishia kumbe kulikuwa na ulazima kupata msaada wa watu wa marekani ili kusema na wenzi wetu....
 
Siri anayo mwenyewe kama kweli anaenda au anaenda kwenye mambo yake still kwenda kwenye mkesha si chanzo cha kusema ameokoka kwani hauwezi kukesha nyumbani kwako unasali

kila mtu anaimani yake, mwanamke huyu anaamini kwenye mkesha anakuwa na muda zaidi wa kuimarisha imani yake, mom bado hajaenda mkesha anaamini hom panatosha pia!
 
Huo sio mkesha ndugu....! Aidha, naye ajaribu mojawapo kati ya haya:

  1. Awe anamsindikiza kwenye mkesha, atamwona jinsi atakavyochokwa na mkewe kwa sababu INFIDELITY kashaingia kati yao...!
  2. Aingie mkataba na muumini mwenzake ili awe anakuja nyumbani kwa siku zile ambazo mkewe anakwenda kwenye mkesha...!
  3. Naye aanzishe mikesha yake, hivyo, kila mkewe akichukua bible kwenda mkesha, basi naye achukue yake na aende zake....!
  4. Atambue kuwa maisha yanahitaji mahesabu makali, lakini hayana fomula maalum, hivyo ajaribu kutumia masharti mazito kidogo ili apate kuona reactions za mkewe juu ya hilo....!
Vinginevyo, aelewe kuwa kinachomtafuna ni INFIDELITY tu, na wala si vinginevyo....! So, fight against INFIDELITY na sio mkesha...!
 
shukuru Mungu ameokoka maana angeamua kuwa sister du ungemfukuza
Sawa kabisa au angeamua kwenda kushinda kwa waganga wa kienyeji je? Mshukuru sana MUNGU wako wife yupo kwenye mstari, hizo starehe haziishi baba na mwisho wake always utaishia kitandani, mara figo mara sijui kisukari mkeo huyo huyo ndo atakayekuwa anakuhudumia
 

:becky::becky: Kweli beijing imekua sana :becky: kwa hiyo mkesha ruksa :becky: hehehe:becky:
 

Beauty, hiyo bado siyo sababu ya kuhalalisha infidelity. amwambie wazi kuwa hapendi hiyo tabia, kama kweli anafanya kwa ajili ya Mungu ataacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…