Hii ndio Habari ya Mji

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,373
SEREKALI TATU!

Watanzania eleweni kua, Chama chochote kinacholazimisha wawakilishi wake kupiga kura ya wazi ili kuwabana kupigia kura SEREKALI MBILI badala yaSEREKALI TATU wanayo itaka, ni chama cha KIHAINI, kwani kinaua Msingi mkubwa wa Demokrasia, Uhuru wa kuchagua bila vitisho(kura ya siri), kwa maslahi ya NCHI yao na sio Maslahi ya Chama, kwa manufaa ya watu wachache.

Kiwekeni alama hicho chama, maana chama chama hicho ndio sababu ya Umasikini wetu katika nchi ambayo dunia nzima wanatamani ingekua yao kutokana na wingi wa rasilimali tulizo nazo.

Jiulizeni hivi, kwani hawa jamaa wana ajenda gani kuzidi maslahi ya Taifa?.

ANGALIZO. (ZINGATIENI USHAURI WA MHESHIMIWA RAIS).

Katika kujadili Rasimu ya katiba, mambo yote ni muhimu, ya angaliwe kwa kina, sio suala la Muungano peke yake (Serekali tatu v/s Serakali Mbili).

Mheshimiwa Rais alitoa Mfano wa Moja ya vipengele katika Rasimu hiyo kua, Sifa ya Kua Rais wa Jamuhuri ya Muungano ni kua Mbunge. Ubunge wa mtu unakoma baada ya Vipindi vitatu. Hivyo basi mtu alie hudumia ubunge katika vipindi vitatu hawezi kua Raisi maana alishakoma kua Mbunge. Hoja kama hizo zinabidi ziangaliwe kwa kina na umakini sana.

Naungana na Rais kua, kuna mambo mengi muhimu ya kuangalia kwa kina katika kupata katiba ilio bora.

Ila hili la Muundo wa Serekali ni Muhimu zaidi pia. Ni kama MOTHERBOARD, katika Computer.
 
Naikaribisha tanganyika kwa mikono yote tanganyika ya baba na babu yangu sasa mtoto anaelekeya kuiona live bila chenga. Punguza jazba yule asieitaka tanganyika usimuite muhaini umekoseya kwani anamawazo yake lakini tunataka tanganyika yetu
 
Kwanini huu muungano ni wakulazimishana, chaa ajabu hata hao tunawalazimisha, wenyewe hawataki.
 
Tuna Tanganyika chamber of commerce, tuna tanganyika lawa society...tuna tanganyika motors, lake tanganyika , tanganyika packers,...etc....ila siku zote tangu nikiwa mdogo sana..nimekuw anikipata shida kuelezea ipo wapi tanganyika yangu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…