joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Si kitu cha kushangaza kuona wakenya wanachanganyikiwa na wengine kupinga kwamba serikali ya Tanzania inaweza kutekeleza miradi mikubwa kwa pesa za ndani, jambo ambalo ni ndoto ya mchana kwa Kenya kutekeleza.
Jambo linalowafanya kushangaa, ni pale wanapolinganisha bajeti kubwa inayopangwa kila mwaka, lakini hakuna linalofanyika, badala yake GoK imekua ikikopa hata kwa miradi midogo sana.
Kitu ambacho wakenya wengi wanashindwa kuelewa ni kwamba, haijalishi ni kiasi gani unapata kwa mwaka, muhimu zaidi ni nidhamu ya matumizi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato.
Hiyo ndio siri kubwa ya mafanikio ya Magufuli katika utawala wake, yeye aliamini kwamba, kama ataziba matobo yanayovujisha na kusababisha upotevu wa Fedha za serikali, miradi mingi inatekelezeka bila mikopo.
Kama Kenya haitoziba hii mianya, hata bajeti ikiongezeka Mara mia moja, Kenya utaendelea kuwa shithole country, kwasababu rushwa nayo itaongezeka Mara mia mbili.