TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Uchaguzi wa serikali za mitaa upo jirani sana, Wagombea kutokea vyama mbalimbali wameanza kujipanga ili waweze kupata ridhaa ya vyama vyao.
Sambamba na hilo pia uchaguzi mkuu ni hapo mwakani tu panapo majaliwa, kuelekea katika chaguzi zote rushwa inatamba sana, wengi hutoa rushwa kwa mifumo nã mbinu tofauti tofauti kulingana na nafasi walizonazo kwa sasa ama umaarufu.
Kulingana na tafiti zangu nilizozifanya, wagombea wengi hutumia viongozi wa chama na serikali za mitaa ili kusambaza rushwa kwa wapiga kura ili wampigie kura muhusika, nimekaa na vijana mbalimbali miezi miwili iliyopita nikiuliza ni kitu gani kinamshawishi ampigie kura mgombea flani?!vijana wengi walijibu,”atakayekuja na hela nzuri ndio huyo huyo”.
Nilipohoji mlishawahi kupewa mara ngapi? Ni kajibiwa kila uchaguzi tunapewa.
Nikaenda ndani zaidi kuuliza je inamaana mgombea anawakusanya na kuwapa hela?
Wakasema hapana Mgombea anaonana na wajumbe wakila shina,anapewa chake kisha anapewa kiasi flani cha fedha kulingana na idadi ya kura anazohitaji na Mara nyingi huwa kati ya 15k-20k, mjumbe anaanza uwapitia wale watu ambao anajua wana dhiki na hawawezi kuchomoa huku akiwatishia kwamba wakila hela nawasipopigia kura wataona.
Njia nyingine ni kupitia mabonanza, kuelekea uchaguzi huwa kunakuwa na mabonanza yanayofadhiliwa hawa na watia nia ama wale waliopo madarakani wanahitaji kuendelea kuakilisha, kupitia mabonanza hayo wahusika huongea na vijana wa timu zote zilizoshiriki kuwa wampigie kura na anateua waratibu wake ambao watahaikisha wengi watamigia kura, huwa wanapewa fedha kiasi akishinda tu kiasi kilichosalia anapewa kiongozi aliyekuwa ameteuliwa nakuwalipa wenzake na huwa wanarudi kufuatilia kupitia ile wanaita wanarudi kuwashukuru wapiga kura.
Kwa muktadha huu ni rahisi kulikabili hili endapo tu ngariba sio diwani wa kata.