Hii ndio nafasi pekee kwa Feisal Salum kucheza soka la nje

Joined
Oct 16, 2015
Posts
20
Reaction score
56
Kuna taarifa zinazomuhusu kiungo wa Yanga Feisal Salum kuhitajika na vilabu viwili nje ya Tanzania. Kwenye email rasmi ya Yanga na CEO kuna ofa mbili za Feisal Salum, kutoka klabu ya Ligi kuu Uturuki na Klabu ya Ligi kuu Misri.

Maoni yangu

Kama kweli kuna hizo ofa mezani huu ndio muda muafaka wa Faisal kutoa nje ya taifa hili ,kwasasa ana umri wa miaka 24 .Hajachelewa sana maana anatoka akiwa amekomaa ..

Bila shaka wengi tulitegemea hilo kutokana na ufanisi wake msimu huu ..amekua mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha yanga ..namba zake pia zinalidhisha .

Binafsi nilikua nikumungalia feisal akiwa uwanjani;roho ilikua inaniuma sana kuona mchezaji mahili kama huyu astahili hata kidogo kuendelea kubaki tanzania . ustadi katika soka ,uwezo,upambanaji na maamuzi ni moja ya wachezaji waliokamilika na kujitofautisha na vijana wengi wa kitanzania .

Ilikua ni lini kumuona feisal hakiitajika nje ,muda ndio huu …hutokea mara chache sana tena nyakati ambazo ndio kwanza umri unaruhusu .

Sioni kama klabu ya Yanga kama wanaweza kuibania ofa hiyo ,maana hakuna wamachomdai feisal ,kilichobaki ni kumlipa fadhila za kumruhusu aondoke ili akakamikishe ndoto,na pia itakua ni faida kwa taifa hili .

Naamini klabu ya Yanga inaviongozi makini sana,licha ya kuwa na malengo mengi msimu ujao kupitia feisal .. lakini ni vyema wakaangalia hili la faisal kwa jicho la tatu maana hakuna watakachopoteza kutokana pia wanae Aziz Ki ataziba vyema nafasi ya feisal .

Naaamini uwezo wa feisal ,pia namuona feisal ikifika mbali zaidi kama endapo ataenda kucheza uturuki ..Feisal Salumu muda ndio huu ukizembea utafuata nyayo kama za akina kaka zako waliokutangulia kwenye soka .

Waliwahi kupata ofa kama hizi wakazipuuzia kwa kujali zaidi mapenzi ya vilabu vyetu na sasa wapo kwenye majuto .. Hutokea mara chahe sana .

Imeandikwa na Nasri Kulemba
instagram nasrikulemba
 
Kuna taarifa zinazomuhusu kiungo wa Yanga Feisal Salum kuhitajika na vilabu viwili nje ya tanzania .Kwenye email rasmi ya Yanga na CEO kuna ofa mbili za Feisal Salum, kutoka klabu ya Ligi kuu Uturuki na Klabu ya Ligi kuu Misri...
Yanga kwa wachezaji ni kama kupe na ngozi. Sidhani kama wanaweza kumuruhusu
 
Kila la heri kwake. Naamini ikija ofa ya kueleweka, na yenye maslahi kwa pande zote 3, viongozi watamruhusu. Ameruhusiwa Simon Msuva, Tuisila Kisinda!

Kwa nini isiwezekane kwa Fei Toto, kiboko ya Aishi Manula na Benno Kakolanya!
 
Kuna jamaa ananong'ona hapa eti Feisal bado,namuuliza kwa nini anajibu umesahau kina Lunyamila na Ngasa.

Nimemwambia aache hizo fikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…