Hii ndio ndege(bomber) hatari zaidi ya kivita duniani

chavalla

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
451
Reaction score
354
Na Josephat K. Nyambeya
B-2 bomber ndio ndege hatari zaidi ya kivita kuwahi kutengenezwa duniani, ndege hii hujulikana sana kwa jina la (Popo) kwa sababu inafanana na popo kiumbo. Ilianza kutengenezwa kipindi cha vita baridi na utengenezaji wake ulitunzwa kwa siri kubwa ambayo haijawahi kuvuja hadi leo. (B-2) ni kifupi cha B-2 Spirit Steath Bomber. Wakati wa kutengenezwa kwake wafanyakazi na wahusika wa kiwanda kilichokuwa kinaitengeneza ndege hii walichunguzwa na kulishwa kiapo cha kutotoa siri , walikuwa wakilindwa na vyombo vya Usalama vya Marekani kwa hali ya juu. Thomas Cavanaugh mmoja ya waafanyakazi alikamatwa kwa kujaribu kutoa siri hii kwa Urusi na alihukumiwa kifungo cha maisha jela japo mwaka 2001 allitolewa kwa msamaha wa PAROLE.
Hadi sasa B-2 ndio ndege vita ghari zaidi kuwahi kutengenezwa duniani, ndege hii inamilikiwa na Jeshi la Anga la Marekani (United States Air Defence Forces /USAF), teknlojia hii na ndege hizi hazijawahi kuuzwa kwa nchi yoyote hata washirika wa Marekani NATO hawajawahi kuuziwa. Kwa sababu ya ughali wake na gharama kubwa za kuiendesha Jeshi la Marekani linasadikiwa kuwa na ndege hizi 20 tu ambazo zinalindwa na kuendeshwa kwenye kambi ya Jeshi la anga ya Whiteman huko Missouri. Ndege moja ya B-2 iligharimu Jumla ya Dollar Billioni 2.1 (kwa rate ya dollar ya mwaka 1997) kwa ajili ya kutengezwa hadi kukamilika.
B-2 bomber haionekani kwenye rada yoyote ile kwa sababu imetengenezewa mfumo wa kuvuruga mawimbi yoyote. Ndege hii ina mfumo wa kunasa na kutambua kila kilichopo ardhini ikiwa huko angani, ina mfumo wa Kushambulia wa Kieletroniki wa kisasa zaidi.
Ndege hii ina uwezo mkubwa wa kubeba silaha za kushambulia ikiwemo mabomu, Makombora, na pia ina uwezo wa kubeba makombora ya masafa marefu ya Nyuklia. Ina uwezo wa kutembea km 12,000 bila kujazwa mafuta. Inaweza beba silaha zenye uzito wa tani 18. Dege hili hatari lina uwezo wa kupaa futi 50,000 juu sawa na mita 15,000.Ndege hii pia inafanya kazi katika mazingira oyote ya hali a hewa na pia usiku na mchana bila kupata matatizo yoyote. Ina uwezo wa kubeba Mabomu 16 ya tani 1.1 kila moja ya Nyuklia na na mabomu 8 ya kilo 230 kila moja ya GPS guided bombs. Ina uwezo wa kupenya katika anga yoyote duniani hata kama ina ulinzi wa kuzuia bila kuonekana, na lengo la kutengenezwa kwa ndege hii ilikuwa ni kuweza kupenya anga ya Urusi na kushambulia maeneo muhimu.

Dege hili lilianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye sura ya dunia mwaka 1989 wakati wa vita ya Ghuba japo halikuhisika kwenye mashambulizi yoyote, tokea kuzinduliwa kwake ndege hii inasemekana imefanya mashambuzi nchini Kosovo mwaka 1999 na kwenye vita ya kumuondoa Sadam Hussein nchini Iraq 2003 na mwaka 2011 kwenye operesheni Odyssey dawn. Inatarajiwa kutumiwa na Marekani kama Korea Kaskazini itaendelea na majaribio yake ya Nyuklia .
Ninaomba msomaji atambue kuwa kuna aina nyingi za ndege za kivita kama Bombers, Jet Fighters, Intercepters , Carriers n.k ila hapa leo ninajadili BOMBERS, siku nyingine nitaandika kuhus Jet fighters.
Baadae yatafuata Maelezo ya Tupolev Tu-160 almaarufu kwa jina la Blackjack kifaa kutoka Urusi..
[HASHTAG]#POST[/HASHTAG] HII KWA HISANI YA
 
Dege hili hata camera haiwezi kupata picha yake!! Kweli au???? mbona hujaweka kapicha??
 
Kwani hii na blackjack ya Russia kuna tofauti gani?,

hii ndege kwanza ni very delicate,inatunzwa kwenye hangar lenye kiyoyozi,
ikipigwa vumbi tu inaknock,
kwasababu hii,inabidi ndege itoke marekani kuja kushambulia mfano iraq ama libya,kwasababu haiwezi hifadhia pengine pasipo na nyumba yake maalumu,
wakati blacjack pamoja na kuwa sio stealth,ina masafa sawa na hiyo,ni kubwa kuliko bomber yeyote kuwahi kuundwa,pia ina missile launching platform ambayo inaifanya isiwe na ulazima wa kuingia anga la adui,kwani inaweza kuwa anga la dodoma,ikafyatua kombora likatua New york,ukubwa wake unaipa uwezo mkubwa wa kubeba silaha nyingi kwa mkupuo mmoja,
 
Kwa wasio ifahamu hii B-2 bomber inataka kufanana na ile F-117 iliyotunguliwa kule serbia,
tofauti ni kuwa F-117 ilikuwa na badass loking kuliko hii B-2 bomber,ingawa imekuwa improved sana kuliko ndege yeyote ya marekani
 
Kwa wasio ifahamu hii B-2 bomber inataka kufanana na ile F-117 iliyotunguliwa kule serbia,
tofauti ni kuwa F-117 ilikuwa na badass loking kuliko hii B-2 bomber,ingawa imekuwa improved sana kuliko ndege yeyote ya marekani
 
Kwahyo zikigongana na B-2 bomber na Blackjack ipi itawahishwa mochuwari[emoji120]
 
Niliwahi kuambiwa hii ndege inaweza ku-outsmart any missile. Je, kuna ukweli ktk hili na inafanyaje kazi?!
Nitoe tongotongo hapo.
 
mkuu mbona huonekani siku hiz
 
Haya ndio maneno sasa, shusheni madude wengine tupo na papcone hapa tunawazumu tu na hayo mavifaru yaliyochangamka yaani🤣🤣🤣
 
Tutainunua lini kwa hela zetu wenyewe bila ya kuwatilia huruma mabeberu?
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…