Hii ndio Ndege ya abiria inayosafiri kwa haraka zaidi kuliko sauti

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Hello JF

Karibia miongo miwili baadaye ulimwengu unakaribia kuwa na ndege ya abiria inayoweza kusafiri kwa kasi zaidi ya kasi ya sauti.

55200303_101-600x338.jpg

Mwezi Huu , kampuni ya ndege ya Boom Supersonic ilianza kufanyia majaribio ndege yake aina ya XB-1 Supersonic.

Ndio ndege ya kwanza aina ya Supersonic ya raia tangu ndege ya Urusi ya Tupolev TU -144 mwaka 1968. Ndege hiyo nyembamba itajaribiwa.

Inatarajiwa kubeba kati ya abiria 65 na 88 kupitia njia za anga ya bahari. Shirika la Nasa lina ndege za kushangaza zaidi zenye mabawa madogo.

Hii itapaa mnamo 2022, ikifuatilia tuzo ya ndege endelevu zaidi.

Pia kuna kamapuni ya kutengeneza ndege ya Aerion, inayosema kwamba aina yake ya ndege itatoa ndege yenye kasi zaidi kufikia mwisho wa muongo huu.

Lakini ikiwa na uwezo wa kubeba kati ya abiria 8 hadi 10 ndege hiyo ya AS2 inalenga soko tofauti ya baishara ya usafiri wa anga za juu .

Mike Bannister aliendesha ndege ya mwisho ya Concorde ya kmapuni ya ndege ya British Airways

Bwana Bannister anasema kwamba ni muhimu kuelewa kwamba ndege hizo hazina upinzani bali ujio mpya katika sekta tofauti ya biashara ya usafiri wa ndege.

Shida moja ya uhandisi ambayo ndege hizi zote zinapaswa kukabiliana nayo ni jinsi zitakavyoingiza hewa katika injini kwa kasi kubwa.

Kuvuta hewa kwa kasi ya hali ya juu kunasababisha matatizo kwa injini zote za ndege.

Uingizaji huo umebuniwa ili kuvunja utiririshaji huo wa hewa na kuipunguza kasi ambayo injini inaweza kukabiliana nayo.

Ni eneo nyeti sana, ambalo hata lilisababisha mgogoro wa England na -Ufaransa wakati wa Concorde.

Kampuni ya ndege ya Air France ilisitisha usafiri wa ndege zake , lakini kampuni ya ndege ya Britrish Airways iliendelea na safari zake.
 
Tupo kwenye uchinjaji ng'ombe kwa dakika therathini.

Wkt aliye panda jeti kwa dakika hizo keshatua mkoa mwingine anakunywa kahawa.

Manbo mengine yanatia hasira sana.
 
Even Concorde was faster than sound...
Kilichowaponza kipindi kile walikuwa wanafanya vitu kwa haraka ili tu bidhaa iingie sokoni,
Madhara yake yalikuwa ni makubwa kupita kiasi, Tupolev TU-144 ndiyo walikuwa wa kwanza kabisa kutengeneza,
Siku wameipeleka Ufaransa kwenye Paris Airshow mwaka 1973 kutambishia dunia bahati mbaya ndege ikaanguka.

Mfaransa na Muingereza nao wakatengeza Concorde lakini nayo ikawa ina matatizo kama Tupolev TU-144,
Ndege ilichinja watu sana mwishowe wakaamua kufunga mradi kwasababu ulikuwa ni gharama sana una madhara.
Wataalamu wanasema ilikuwa inapiga kelele, inachafua mazingira na kumwaga baadhi ya vitu vinavyosababisha kansa.

Marekani anaweza kufika mbali kuliko Mrusi, Mfaransa na Muingereza kwasababu yeye amepata muda mwingi sana kujiandaa na huu mradi wa Super-Sonic Jet. Mwaka 1990-1999 wanasayansi wa NASA walikuwa wanatumia ndege za Urusi Tupolev TU-144 katika kufanya majaribio ya kutengeneza Super-Sonic Jet ambayo itakuwa ya abiria.

Sasa ukiangalia kiwango cha pesa ambacho Marekani wanacho na ujuzi walioupata kutokana na kuisoma miradi ya Super-Sonic Jet ya Urusi kwa miaka mingi: Kuna uwezekano mkubwa sana huu mradi unaweza kuwa wa aina yake.
 
Warusi wana bahati mbaya. Walitoa Sukoi super jet test commercial flight ya kwanza nafikiri Malaysia ikala mzinga(pilot error) tangu pale ikawa mkosi kwenye mauzo.
 
They work under extreme pressure, with a somber cloud of limited resources.
Ukichanganya siasa na hujuma, sidhani kama itakuwa rahisi kwa ndege za Urusi kufanya vizuri sokoni.
 
ภץเє รเ ๓к๏ ๒ยรץ ภค кยɭค кเ๓кคкคՇเ..คย кเ๓ครเђคгค..ץєภย ภเ ђคץ๏ Շย!
 
Concorde ilikua ina kas mara mbili zaid ya kas ya saut
Kwahyo ni marudio tu hayo
 
Kilichowaponza kipindi kile walikuwa wanafanya vitu kwa haraka ili tu bidhaa iingie sokoni,
Madhara yake yalikuwa ni makubwa kupita kiasi, Tupolev TU-144 ndiyo walikuwa wa kwanza kabisa kutengeneza,
Siku wameipeleka Ufaransa kwenye Paris Airshow mwaka 1973 kutambishia dunia bahati mbaya ndege ikaanguka.

Mfaransa na Muingereza nao wakatengeza Concorde lakini nayo ikawa ina matatizo kama Tupolev TU-144,
Ndege ilichinja watu sana mwishowe wakaamua kufunga mradi kwasababu ulikuwa ni gharama sana una madhara.
Wataalamu wanasema ilikuwa inapiga kelele, inachafua mazingira na kumwaga baadhi ya vitu vinavyosababisha kansa.

Marekani anaweza kufika mbali kuliko Mrusi, Mfaransa na Muingereza kwasababu yeye amepata muda mwingi sana kujiandaa na huu mradi wa Super-Sonic Jet. Mwaka 1990-1999 wanasayansi wa NASA walikuwa wanatumia ndege za Urusi Tupolev TU-144 katika kufanya majaribio ya kutengeneza Super-Sonic Jet ambayo itakuwa ya abiria.

Sasa ukiangalia kiwango cha pesa ambacho Marekani wanacho na ujuzi walioupata kutokana na kuisoma miradi ya Super-Sonic Jet ya Urusi kwa miaka mingi: Kuna uwezekano mkubwa sana huu mradi unaweza kuwa wa aina yake.
Mi nadhani hata hiyo inaweza kufail kama hawatapambana na kupunguza running costs,kwani mashirika ya ndege yanachoangalia zaidi ni faida,unaweza kutengeneza ndege kubwa sana kama Airbus A380 au yenye speed kubwa kama hiyo Tupolev lakini inapokuja kwenye biashara inakuwa ni hasara,kwahiyo utakuta mashirika mengi hayatainunua kwa kukwepa hasara...
 
we mzee unajua kwamba concord ilikua inasafiri at MACH 2.04 yaani zaidi ya mara mbili ya speed ya sauti?
Karibia miongo miwili baadaye ulimwengu unakaribia kuwa na ndege ya abiria inayoweza kusafiri kwa kasi zaidi ya kasi ya sauti.
 
Concorde ilikua inakwenda speed ya Mach 2.04, yaani zaidi ya mara mbili ya speed ya sauti.

Kwahiyo siyo jambo jipya, labda kama lengo lao ni kuifanya iwe more economical na isiyo sababisha makelele mjini kama ilivyokua concorde.
 
Mwaka 2000 ilipokuja Cape Town ilitangazwa sana kwenye TV na pia wengine tulipewa ruhusa kazini hiyo siku tukaishangae ilikua jumanne ya February 16 siji kuisahau mimi nilikua sijui Mambo ya ndege kabisaa ila kufika hapo uwanjani kulikua na watu wengi mno nikagundua inawezekana ni kitu tofauti wacha niende karibu nikaulize na maswali kwa wataalamu...baadae nikaja kusikia imepata ajali ufaransa nilisikitika sana maana nilikua nishaanza kuifatilia na nilisema ipo siku ntaipanda maana ilikua inatumika masaa nane na dk kadhaa kutoka cape mpaka UK wakati 787 iliweka rekodi ya kutumia masaa 11 na dk kadhaa...
 
Mi nadhani hata hiyo inaweza kufail kama hawatapambana na kupunguza running costs,kwani mashirika ya ndege yanachoangalia zaidi ni faida,unaweza kutengeneza ndege kubwa sana kama Airbus A380 au yenye speed kubwa kama hiyo Tupolev lakini inapokuja kwenye biashara inakuwa ni hasara,kwahiyo utakuta mashirika mengi hayatainunua kwa kukwepa hasara...
Naamini hii ndege itakuwa ni ghali sana ikiisha ingia sokoni: Marekani atataka kurudisha fedha za tafiti.
Ukizingatia kwamba hii ndege ni New Generation of Civilian Aircraft, basi Running Cost lazima itakuwa ni kubwa sana.

Sema hatari ni kwamba teknolojia na tafiti zilizotengeneza hii ndege zinaweza kufika mikononi mwa Uchina siyo muda,
Yeye atafaidika kukwepa Trial & Errors of Scientific Research ambazo NASA watapitia nakuiweka ndege kwa bei poa.
 
Wacha wahangaike huko, sisi tupo na vumbi la congo kwanza.......
 
Back
Top Bottom