Hii ndio njia iliyobaki kujikwamua na umasikini kwa sisi watoto wa kimasikini

October man

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2017
Posts
3,635
Reaction score
5,012
Habari wana jukwaa ni maatumaini yangu kuwa ni wazima, niende moja kwa moja kwenye mada, kiukweli kwamba asilimia ya watu wengi maisha ni magumu ila moa ya tatizo linalotukumba wengi wetu ni kutokuwa na mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara ili kujikomboa katika hali hii mbaya ya kiuchumi au muda mwingine kukosa kabisa mtaji mzima, mtaji umekuwa ni serious problem haswahaswa kwa vijana ila mtaji utaendelea kwa ni tatizo vizazi na vizazi endapo watu tutashindwa kuwacha ubinafsi na kuwa pekeyake pekeyake, umoja na ushirikiano ndio njia rahisi ya mafanikio kwa dunia ya sasa hivi kwa sisi watoto wa kimaskini, kwa kupitia umoja na ushirikiano tunaweza tukafanya project kubwa kubwa, biashara na uwekezaji mkubwa na hatimaye kufika mbali kumiliki kampuni zetu wenyewe.

kwa mfano tu wanachuo munaosoma pamoja na kupokea boom kikweli boom ni pesa ndogo sana mpaka ukimuona mtu kanunua hata laptop hakununua kirahisi rahisi kuna action alifanya, sasa tunapokuja kwa wanachuo kupata mtaji wenye tija na unoleweka wakufanyia project frani inakuwa ni ngumu ila linapokuja suala la kuwa pamoja na kuunganisha nguvu mtaji mkuwa huwa rahisi sana kupatikana ila hili waliowengi hawalioni wanaishia kuwa selfish tu.

kampuni nyingi za kichina zimezaliwa kutokana na kuunganika watu hata mia na kuwekeza kwa pamoja kwa uwekezaji wa muda mrefu, mpaka leo wana mafanikio makubwa sana na makampuni makubwa mengi sana ila ukija kwa watanzania kila mtu kaikumbatia pesa yake ndogo ndani.

hivi imagine undapo mutaungana watu hata kumi kila mtu aka weka million moja ambayo itakuwa sawasawa na million kumi arafu muka wekeza kwenye biashara ambazo zina tija kama kilimo au na investment yoyote na mukapata profit mukawekeza kwengine mukapata faida mukawekeza tena kwahiyo mwisho wa siku muna investment hata nane au kumi na inakuwa rahisi kuzi manage kwasababu muko wengi na kila mtu atachukua majukumu yake mwisho wa siku mnakuwa na hata makampuni yenu ila sasa unakuwa pekeyako na ka million moja chako na ubinafsi na kutaka faida za haraka utaishi chini juu utaendelea kuwaona wakina Mengi, Mo na Bakhresa ila tutapoungana kwa pamoja tutaweza kufanya ushindani na wakina Mengi.

hapa naongea ana watoto wa maskini kama mimi inabidi tuamke sasa muda ndio huu maisha yanavyozidi kwenda ndio changamoto zinazidi ni kweli wazazi wetu walikuwa maskini inafikia hatua mzazi anashindwa kukupa hata laki tatu ya ada tu mpaka vikao vikaliwe wakope fedhea na kadharika nisingependa turuhusu hili litokee kwa watoto wetu sisi ni muda wa kuwa na mawazo ya makampuni sasa.


NB: uwekezaji wenye tija ni ule wa muda mrefu sio ule faida za leo kesho, pia mungu hubaliki katika umoja na ushirikiano

NAWASILISHA

OCTOBER MAN
 
Umoja ni nguvu!
Huku kazini kwetu kuna watu baba mmoja mama mmoja hela ya sukari robo 650 wanashindwa kujichanga matokeo yake kila siku kazi kuomba watu sukari ya chai.Sasa unadhani watu wa sampuli hii wanaweza kuungana na kujichanga mtaji wa milioni moja ili wajikwamue na umasikini?
[HASHTAG]#Tatizoubinafsi[/HASHTAG]
 
Hili wazo ni zuri na siyo geni,sema vijana wa kibongo tunaishia kupanga,utekelezaji zero, mimi pia napenda ushirikiano kama huo
 

millioni moja ni mfano hii inamaana mutaungana kulingana na hali zenu mfano kwa wanafunzi chuo wanuwezo wa kujibana kupata million moja nakuunga kwa pamoja hivo hivo kuna watu wanuwezo wakuunganisha million kumi kumi nk, kwahivyo hata awo wanaweza kufanya strategy zitazowaingizia kipato na kuunga hata elfu hamsini hamsini, kingine wanawezaje kuomba pesa watu kwa kwaajiri ya kitu ambacho sio basic wanaweza kula vitafunio bila chai tu ingekuwa wanaomba pesa ya chakula basic kama ugali kweli ila sukari kwaajiri ya chai ni starehe ikiwa uwezo hauna
 
Mawazo mazuri, lakini kuunganisha nguvu kama hivyo unavyotaka wewe sijui kuwa na kikundi cha watu wala haijalishi unaweza kuunganisha nguvu hata na mtu mmoja tu na wewe ukiwa kama mtu wa pili na kila kitu kikaenda sawa. Tatizo watu wenyewe siku hizi hawaaminiki, utapeli na ujanja ujanja miongoni mwa watu imekuwa kama jambo la kawaida sana. Wakati mwingine mtu anaona ni bora ajitenge abaki na chake hata kama ni kidogo . . . Inahitaji umakini, uaminifu na akili ya ziada kuunganisha nguvu na mtu, au kikundi cha watu.
 
Biashara kamaa hii imeniingiza mkenge mwaka jana , business partner Wangu kaingia tamaa nikapata loss ya 6450,000/= akafirisika mazima. Mambo haya tuwaachie wahindi na wachina.
 
Nikweli kaka edwin kuwa bussiness partener yahitaji muwe kwanza mshachunguzana kwa zaida hata ya miaka10 na ushuhuda nabiashara ya mzee yuko partner najamaa flan hivi alikua anamuuzia mizigo baada ya miaka18 ndo amewez kua partner anapewa mzgo wa mali kauli hata milioni100 baada yakua amejenga uaminifu wahali yajuu kwa zaidi ya miaka18
 
Hahahaha watakuwa walimu nn?
 
Mkuu umenena sawia kabisa, tatizo sio kuungana tatizo lipo kwenye uaminifu wabongo wanapenda utapeli kuliko kula. Bora niwekeze kivyangu ntakapofikia basi nimushukuru mwenyez mungu. Wabongo nomaa sana kweny hela.
 
Mada imenigusa sana hii na inanihusu sana mtu kama mimi.

Mimi huwa nasemaga kila siku kwa mazingira na maisha ya kitanzania kwa ujumla ni vigumu sana mtu yoyote kufanikiwa kutoka chini bila kupata ushirikiano wowote ule hasa kwa mtu anaetoka familia masikini, ni vigumu kutoka bila kuvutwa na shati.

Nchi yetu iko very corrupted na msaada wake ni kwa wanainchi ni kidogo sana kulinganisha na nchi zilipoga hatua, nchi zilizopiga hatua mfano kwa hapa Afrika South Africa wananchi wake hasa masikini wanapata unemployed benefits kwa ajiri ya kuwalea wazee na watoto wasiwe omba omba(beggers) pamoja kupunguza dependency ratio na pia vijana wanapewa funds bila vikwazo kukuza entrepreneurship skills hili siku za mbeleni waje wawe na wawekezaji wengi wa ndani na sio eti 96% wa wawekezaji wawe wanatoka nje kama hapa.

Sasa kwa Tanzania yetu hii hayo yote hayapo, nchi masikini aileweki na bado serikali haiwajari raia wake raisi anasimama bila aibu anasema kabisa "kama hamna chakula mfe tu". Na bado tulio wengi tumetawaliwa na ubinafsi kwenye nafsi zetu, kiukweli hapo maisha lazima yawe magumu sana na vibaka wawe wengi.

Binafsi naamini sana kwenye kusaidiana na nna uhakika 80% ya watu waliofanikiwa hapa bongo ni lazima wamewahi kushikwa mkono mahali katika safari yao hata kama ni kwa muda mfupi tu. Hizi stori za kuwa self-made millionaire bongo ni kudanganyana tu kwa mazingira yapi kwanza?

Kikubwa kinachotuangusha ni uaminifu tu, mimi naamini kuna vijana wana access na hela za mitaji ila hawajui wazifanyie nini na pia kuna vijana wana idea kibao tu lakini hawana hata 100. Kama hawa wawili wakikutana na wote wakawa waaminifu I am sure watapunguza umasikini kwenye familia mbili na kuendelea.

Ushirikiano ulio na nidhamu ndio nguzo pekee kwa vijana masikini angalia wasomali jinsi wanavyotoana kwa misingi hii hii ya kushirikiana na miaka sio mingi wataushika uchumi wa kusini mwa jangwa la Sahara. Wakati huo wajukuu zetu watakuwa wanatumika kama manamba kwenye miradi yao, wakati hata sisi tukiamua tunaweza kwenda nao sambamba kama tukiamua
 


umeeleza vizuri boss, umoja ni moja ya kitu kizuri ila tatizo wengi wetu hatuna muwamko wa jambo kama hili mfano mimi nili propose kwa wenzngu nilomaliza nao shule hakuna hata mmoja aliye respond kwakeli kutokea hapo sikuona umuhimu wa kuwa nao, nimejaribu kuwa expose watu wangu wa karibu mara mbili bado inaonekana kila mtu mbinafsi mpaka sasahivi watu wamekuwa wabinafsi mno kukosa muamko katika mambo ya kimaendeleo, mpaka nikajisemea bora ukiiona fursa au ukiona kuna matumaini makubwa katika kitu furani chenye tija ukiiendee tu pekeyako, utakapo pata matokeo ndio watajua, kiukweli watu awana muamko kabisa na suala zima la maisha, kutokuaminiana na uaminifu ni moja ya changamoto tu kwasababu katika jambo lolote lenye tija changamoto ni kitu cha kawaida na kwenye safari hii ya mafanikio muhimu kuwa risk taker, endapo mungu atajaalia mukawa waaminifu nauwakika mutafika mbali tu kimaisha.

niukweli usiopingika kwamba njia rahisi ya kumiliki investment kubwa na kampuni ni kupitia umoja ila akiwa kila mtu kivyake kwakeli utasota msoto si wakawaida ni vyema tuiniane katika wengi kuna mengi kila mtu na ujuzi wake, uzoefu mawazo na hekima zake lakini pia kupitia kuwa pamoja inakuwa rahisi kupata hata misaada ya kifedha kwa wadau mbalimbali.

huu ndio muda, kwa kupitia sera za raisi za kufanya kazi na viwanda ni njia rahisi ya kuwezeshwa mtaji wenu ukawa mkubwa mfano juzijuzi tu kuna watu furanini walikuwa wanataka kufungua kiwanda cha matofari wamepewa eneo kubwa na serikali magwepande huu ndio muda wa kuinuana.
 
Aliye tayari tuungane faster. Tuwe 20 tu waaminifu.
 
Walio tayari 20 tu waaminifu tudhubutu basi.
1. Mimi hapa
 
Kuna mtu humu alikuja na wazo kama lako, mpala ilifikia hatua ya kufungua kampuni ya kilimo. Mpaka bank account ya company ikafunguliwa na uchaguZ ulifanyika very fair kuchagua viongoz.


Nakumbuka mikutano ilikuwa inafanyika hapa dar na vijana kutoka mikoani walikuja.


Mwisho wa siku aliekuja na wazo kama wewe alikuwa ni TAPEEEEEELI na MWENYE TAMAAA
 
Mawazo mazuri endapo mkikutana wote mna akili zinazofanana, na muwe na background nzuri. Naweza sema mzee wangu na ndugu yake hawakuwa na mawazo sawa ktk mambo ya kuungana na kufanya kitu pamoja, hali iliyopelekea biashara zao kufa. Mzee wangu amekuwa akikataa kabisa suala la kufanya projects pamoja. Hilo ndio jambo linaloniogopesha kila siku kuungana na kufanya projects pamoja!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…