Hii ndio sababu forex trading inaonekana ni utapeli kwa jamii

Dkt Guston

Senior Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
105
Reaction score
119
Habari wana jamii forums

Kuna baadhi ya watu wanaifanya fx industry kuonekana kama ni kitu scam,kumbe ni wajinga baadhi ambao ni walala hoi wanaifanya hii game ionekane ni wizi,wanajifanya ni mamentor wakati ni wachoma account wazuri,wauza signal za bukubuku,wana ibia watu hela wakijifanya ma agent kumbe hamna lolote

Kuna baadhi ya watu wanajifanya ni wafanya account management za watu wakati zao zimewashinda wamechoma,wanachukua nusu ya wateja wao wanawambia wa buy nusu wanaambiwa sell watakao win wanapostiwa,kwamba good signal waliochoma wana wa block[emoji15]

Waliowin watavuta watu wengine tena,wanapigwa na walipigwa wanatafuta wa kuwapiga, mwisho watu wanaona ni kitu cha wizi

Kama wewe unatengeneza $10000 kwa siku za nini uombe $20 za watu,kwa nini uuze signal za bukubuku nakujifanya kwamba unatoa kwa jamii[emoji23][emoji23][emoji23] mbona John leyks yeye alikusanya watu 100 ambao hawajui forex akawafundisha Bure na akafund account zao huyo ndo alitoa kwa jamii sio nyie wauza signal $75 sijui $100 hafu mnawambia watu ni lifetime baada ya mwazi mnawambia bando lime expire hivi lifetime inakuaje expired[emoji23][emoji23]


Guys acheni kuibiwa kijinga kama mtu amekwambia BTMM & ICT anakufundisha kwa $50 kwa nini usichukue $5 ukanunua MB GB64 ukajifunza serious youtube mbona kuna course nyingi tu huyo anayekuomba $75 na yeye anaangalia YouTube hafu anakuelekeza wewe anajifanya mentor waulize hao traders wenye mwaka hata mmoja kwenye game wale mentors wao bado wana wasiliana nao,yule muuza signal wake bado ananunua,na yule mfanya account management wake bado anamfanyia management[emoji23]

Hii kitu imejaaa matapeli wengi sana wazee wa showoff wakijifanya wamefanikiwa kumbe ni walalia mihogo na maji ya kandolo

Guys achaneni na hao matapeli ,tumia mda wako kujifunza youtube,udemy,discoard utajifunza vitu vingi kuliko hao wezi wanaojifanya wanatoa kwa jamii kumbe hamna lolote,

Msije Sema najifanyia promotion Mimi siuzi signal,sifanya account management, sifanyi mentorship yoyote,nilijifunza fx mwenyewe youtube,TL,discoard nimesoma PDF za kujilisha ubongo vizuri sijawahi kulipia class yoyote kwa hio hata wewe unaweza kuifanya youtube kua mwalimu wako,mtoa signal wako,mfanya account management wako

""ALL WE GONNA MAKE IT""
 
Mtu kama sir Jeff anashinda kwenye majengo na hoteli kwa pesa za kutapeli na kuwauzia watu signal mbovu ndio maana hanenepi na anafake furaha .......!

Huwezi kuwa na furaha hapa duniani kwa pesa za wizi ....
 
Wewe gemu lako likoje mpaka sasa? Umefaidikaje na hii Forex mpaka sasa?

Asante kwa kusema ukweli. Hii kitu inahitaji elimu sana tena bila kukoma. Nilisoma tuvitabu tuwili tutatu nikaijaribu nikala za uso nimerudi tena darasani Youtube na kwingineko.

Na ushauri wangu ni ule ule - kwenye forex, kama kwenye uwekezaji mwingine kwingi kwingineko, weka fedha ambayo uko tayari kuipoteza!
 
Na wewe ni trader
 
Mtu kama sir Jeff anashinda kwenye majengo na hoteli kwa pesa za kutapeli na kuwauzia watu signal mbovu ndio maana hanenepi na anafake furaha .......!

Huwezi kuwa na furaha hapa duniani kwa pesa za wizi ....
Sawa kiongozi
 
Huo ndo ukweli eti wana hisa kwenye mabasi machalii washamba kimbwa

Daily kujifanya motivational speaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…