Tetesi: Hii ndio sababu kubwa ya Marais Wanaong'ang'ania madaraka!

Tetesi: Hii ndio sababu kubwa ya Marais Wanaong'ang'ania madaraka!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Mfano wa hawa binadamu tusiende mbali sana tubaki humu humu mwenye bara letu ambalo wale ndugu zetu waliita "BARA GIZA". Hili neno kwangu hua linaniumiza sana kila ninapolisoma au kulisikia likitajwa mahali popote pale,lakini practices zetu ndio zinasadifu neno husika.Anyways, turudi kwenye mada husika,


Hawa viongozi sababu kuu zinazowasukuma kuendelea kung'ang'ania madaraka ni kujiona kua wao ndio Miungu watu, kwamba hakuna wa kufanana nao kabisa,wao ndio wenye vipaji pekee vya kuongoza na kua wakiondoka madarakani mataifa yao yanaparanganyika, na wanajiwekea mifumo itakayowalinda wao na hufikiria kua akija kuongoza kiongozi mwingine basi mifumo hiyo itaharibika kwa imani zao.Hiki ndicho kinachowafanya kuendelea kubadili katiba za mataifa yao kujiongezea muda wa kuendelea kuongoza japokua nchi zao zinabaki kua maskini kutokana na mifumo yao ya kiutawala amabayo hawataki kukubali wakiambiwa ni mibovu. Itazame Zimbabwe, itazame Uganda,Rwanda,itazame DRC na Burundi. Hizi nchi zote viongozi wake wanaami kua hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuongoza nchi zao zaidi yao na kila anayeonekana kupinga mifumo yao ya utawala wao na kuitwa mchochezi na anatumiwa na wazungu. Yaani kila anayepinga watawala ni mchochezi na anatumiwa na wazungu, serious? Swali pekee kwa viongozi hawa, Je,hawatakufa? Wana mkataba na Mwenyezi Mungu ili waishi milele? Wakifa ataongoza nani? Je,wako wapi Kina Farao,Hitler na Abacha,Mau?

Hakuna haja ya kuuuliza kwanini nchi za wenzetu ambazo tulikua kwenye usawa wa umaskini kama vile Malaysia, India,Brazil na zinginezo ni kwa nini ziko kwenye ulimwengu mwingne?.Sababu kubwa ni kwamba wenzetu hawa walikubali kuheshimu katiba zao, walikubali kuheshimiana na kuona kila mmoja anao uwezo wa kuliongiza taifa lake.

Rai yangu kwa Watanzania,

Ni imani yangu kua hili suala la kujitokeza kwa watu wa aina hii ni ngumu, tulishazoea kuendesha mambo kwa mijibu ya katiba tuliyonayo na tunaiheshimu vyema. Lakini watu. walishaanza kutaka kuwafanya watanzania waamini kama walivyoaminishwa wananchi kutoka kwenye nchi zisizoheshimu katiba, tumekua na vigugumizi kwenye upatikanaji wa katiba mpya lakini tamaa zetu zisitupelekee kufanya hivyo kwa malengo ya kuwaongezea watu muda kubaki madarakani.Tuwapuuze wanaotaka kulianzisha vugu vugu hili maana hawa ndio wanaweza kua ndio wachezi wakubwa na ndio wanaotumiwa.Tujione kua sote ni binadamu wenye haki sawa na hata siku ya mwisho kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake.Wasitake kuliandika historia mbaya taifa taifa letu.
 
Back
Top Bottom