Hii ndio sababu ya ualimu kukosa heshima Tanzania.

Annuity

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Posts
338
Reaction score
198
​Kwa miaka ya hivi karibuni, fani ya ualimu Tanzania imekuwa ikionekana kama chaguo la wakosaji, yaani mtu anakuwa mwalimu baada ya kukosa kazi bora ya kufanya. Lakini kwa siku za nyuma ualimu ulikuwa ni kama lulu, watu walikuwa wanapata heshima kwa kuwa walikuwa ni walimu. Mshara ulikuwa ni mkubwa kulingalinganisha na baadhi ya taaluma na kazi fulan fulan ambazo kwa sasa zinaonekana kama ‘hot cake’. Katika kitabu cha Bwana Olotu Abubakar Olotu alichokiandika mwaka 1971 kuhusu historia ya TANU aligusia jinsi serikali ya kikoloni ya wakati ule ilipomshangaa Mwalimu J.K. Nyerere kwa kuacha kazi ya ualimu yenye mshahara bora na kwenda kwenye kazi ya ya siasa (alipoamua kujiunga na TANU) ambayo ilikuwa na malipo finyu. Nanukuu “Serikali ilikuwa ikifikiri kwamba, ilikuwa jambo la kioja sana iwapo mwafrika mwenye kazi nzuri (ualimu) na ambayo ilikuwa na mshara bora angaliweza kukata shauri la mwisho na kuanza kazi ya siasa ambayo haikuwa ikitoa mshahara wowote wa maana” mwisho wa kunukuu.

Japo nimesikia watu wengi wakisema ualimu hauna hadhi tena hauna mafao mazuri sababu serikali inachagua watu waliofeli wawe walimu. Swali la kujiuliza ni kweli serikali inachagua watu waliofeli wawe waalimu? Na kama ni kweli kwanini serikali ifanye hivyo? (majibu yanahitajika), Lakini kama watu waelewa tunajua hakuna nchi ambayo imeendelea pasipo kuwekeza kwenye elimu na ndio siri pekee ya ya nchi kuwa na uchumi imara. Lakini ni kitu gani kimeisibu Tanzania mpaka mwalimu ambae ni mdau mkubwa wa elimu badala ya kupewa ‘VIP-treatment’ anaonekana kama mtu aliyokosa kitu cha kufanya?

Hata mtoto mdogo akifanya utafiti wa haraka haraka atagundua mchawi wa fani ya ualimu hapa nchini ni wananchi wenyewe kuingia kwenye mkumbo wa kuibeza fani hiyo kwa kutojua mwalimu ana umuhimu gani katika maisha yao y akila siku na kwa kufikiri kuwa wanasiasa ndio wakombozi wao! Lakini ni miaka karibu 40 wanachi hawajazinduka toka usingizini kuwa mwanasiasa kwake sio chaguo sahihi licha ya maisha yao kwenda kombo kila kukicha… ila kibaya zaidi na waalimu wenyewe kutokujitambua na kuona wana umuhimu gani katika nchi kwa kufanya kazi kwa uoga kila wanapotishwa na wasiasa ambao miaka ya nyuma ‘watoto wa mjini wanasema walikuwa wanasubiri kwa waalimu’ na pia waalimu hao hawajui ubora wa maisha wa watanzania katika kipindi cha miaka 50 ijayo ipo mikononi mwao ila wanasiasa wameshika hatamu na waalimu wanaishi wamempoigia magoti mwanasiasa.

​Tukiona Uchina ipo vile licha ya kuwa nao sawa kiuchumi miaka ya 60 inabidi ujiulize nini walifanya na sisi nini tunafanya? Tukiona Malysia ipo vile licha ya kutajwa sambamba na sisi kama nchi masiki kipindi hicho inabdi ujiulize walifanya nini na wanaendelea kufanya nini mpaka sasa hivi tunakimbilia kwenda kusoma kwenye nchi yao? Acha wanaojua umuhimu wa elimu na walimu waendelee kukujengea barabara na madaraja, acha wanaojua umuhimu wa elimu waendelee kukuchimbia madini yako mwenyewe licha ya Mwalimu kusema yaachwe mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kiyachimba, acha wanaojua umuhimu wa elimu weendelee kuifanya nchi yako kama dampo…
 
Nimekupata mkuu...umepresent mambo ya msing sana kwa mustakar wa elim hapa nchin.
 
Wanasiasa ndio wanakwamisha maendeleo ya nchi, wanapokuwa mjengoni wanalipana posho wanazotaka wao, walimu tunakula vumbi la chaki lakini ujira kiduchu! Hembu fikiria mbunge anakusanya zaidi ya mil 10 kwa mwezi akiwa na elimu ya darasa la saba, mwalimu mwenye shahada unampa laki 5 kwa mwezi! Hilo sio tusi? Kwanini bora usimpe mil 2? Kuliko kumdharirisha kiasi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…