Hii ndio thamani ya popi,wahehe washafanya yao.

Hii ndio thamani ya popi,wahehe washafanya yao.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
THAMANI YA POPI.

1)Tumeirudi miaka,ile tisini na ine
Anathaminiwa paka,na wale watu wengine
Tumeiruka mipaka,tumenda pande nyingine
Ya binadamu thumuni,thamani ya popi kubwa


2)Utu wazidi ponyoka,ni dhambi kubwa pengine
Wamsujudia nyoka, awe ndo Mungu mwingine
Sidhani tutanyooka,tusipotenda mengine
Ta binadamu thumuni,thamani ya popi kubwa.

3)Haswa kwa anaebweka,kweli mijitu mingine
Akili zimebweteka,kwa hili acha wanune
Kunapo kukurupuka,vipi akili wakune
Ya binadamu thumuni,thamani ya popi kubwa.

SHAIRI- THAMANI YA POPI
MTUNZI- Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com.
 
Back
Top Bottom