Hii ndiyo Katiba Pendekezwa itakayopigiwa kura nyingi sana za Ndiyo!!!!!!!!

Hii ndiyo Katiba Pendekezwa itakayopigiwa kura nyingi sana za Ndiyo!!!!!!!!

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
Inaheshimu Uhuru wa imani ya dini, Soma mwenyewe Ibara hii ya 41.

41.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni
huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.

(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya Serikali.

(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya utaratibu

utakaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.

(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa
kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.

(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa
wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba
maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
 
Back
Top Bottom