Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Je umefanya maamuzi ya kufikia uhuru wa kifedha kupitia majengo ya kupangisha?. Je umefanya maamuzi ya kustaafu mapema zaidi kupitia majengo ya kupangisha?.
Je upo tayari kuanza kumiliki majengo ya kupangisha ukiwa unaendelea na ajira yako?. Je upo tayari kuanza kumiliki majengo ya kupangisha ukiwa unaendelea kukuza biashara yako?.
Kama ni jibu la maswali yote haya ni NDIO, endelea kusoma ukurasa huu. Nakuhakikishia kuwa hutajuta kutenga muda wako wa thamani sana.
Somo la leo hii: Kutambua lengo kuu la kufanya maamuzi ya kustaafu mapema. Huwezi kufika usipojua unakwenda.
Ili uanze kumiliki nyumba za kupangisha ukiwa bado umeajiriwa unahitaji kufahamu mambo yafuatayo kwa ndani zaidi;-
Moja: Kwanini kubwa.
Pili: Malengo makubwa.
Tatu: Mbinu bora.
Nne: Tabia za kiwekezaji.
Mambo haya unatakiwa kuyafahamu kwa kufuata mlolongo nilioandika hapo juu.
Kwa leo hii, ninakushirikisha kuhusu kwanini kubwa na malengo makubwa.
(a) KWANINI KUBWA.
Ili uweze kumiliki nyumba za kupangisha ukiwa kwenye ajira unahitaji mambo mawili. Moja ni maarifa sahihi ya nyumba za kupangisha na pili roho imara (strong spirit) ya kuhitaji kumiliki nyumba hizo.
Unaweza kuwa na maarifa sahihi na usifikie kwenye kumiliki nyumba za kupangisha kwa sababu una roho (imani) dhaifu.
Maarifa sahihi yanajengwa na kujifunza kuhusu nyumba za kupangisha. Roho (imani) huimarika zaidi unapozidi kujifunza bila kukoma.
Lakini huwezi kutumia maarifa sahihi uliyonayo yahusuyo majengo ya kupangisha kama hutakuwa na imani kubwa ambayo husukumwa na kwanini kubwa.
Mfano; wengi sana katika jamii zetu wanafahamu kuwa majengo ya kupangisha yanalipa. Wengine wakachukua maamuzi ya kusomea digrii (shahada) ya uwekezaji katika ardhi na nyumba na fedha, lakini kwa kukosa na kwanini kubwa waliishia kumiliki nyumba mbili au tatu za kupangisha.
Wanaopata mafanikio kidogo sana wanakuwa na imani dhaifu. Hapa nina maana hawawezi kuona wanamiliki nyumba za kupangisha kufuatana na maarifa waliyonayo.
Wanakuwa na maarifa sahihi lakini wanavutwa na fikra za kukutana na chanagamoto. Ukiwa na kwanini kubwa, unakuwa umejitoa kwa lolote linaweza kutokea.
Wakati huohuo ukiendelea kutumia maarifa sahihi ya nyumba za kupangisha. Ukiwa na imani kubwa ya kupata mafanikio makubwa kupitia nyumba za kupangisha bila kutafuta maarifa sahihi, utachelewa sana kufanikiwa na pengine usifanikiwe kabisa.
Kwanini kubwa ni kunganishi kati ya maarifa sahihi ulinayo na nguvu ya pekee ambayo wanadamu tunaitegemea (Mungu wa mbinguni).
Kulingana na imani yako unatakiwa kuunganisha maarifa sahihi na nguvu itendayo maajabu. Kila mtu anayo nguvu hii. Kwa kufanya hivi, hutaweza kukata tamaa kamwe.
Kwako utakuwa umehsindwa siku unayoingia kaburini. Ifuatayo ni mifano ya kwanini kubwa unayoweza kuwa nayo. Kuajiriwa ni chanzo cha changamoto nyingi kwa walio wengi kutokana na sababu tofauti tofauti.
Moja; imani (dini).
Wengi hushindwa kuwa karibu na Mungu wao kwa sababu ya kanuni na taratibu za kazi. Hii kwa inakuwa ni KWANINI KUBWA kiasi kwamba hawapati usingizi. Kila mara hufikiria kujinusua kwenye mtego huu. Na njia ambayo hufikiria ni kumiliki nyumba za kupangisha ili kuachana kabisa na ajira yao.
Pili; Upendo (familia, watoto na jamaa).
Hawa nao hukosa kabisa amani moyoni mwao kwa sababu ya kukosa muda wa kuonyesha na kujenga upendo ndani ya familia zao.
Migogoro mikubwa kati ndoa yao inasababishwa na changamoto za ajira zao. Hii inakuwa ni KWANINI KUBWA kwao. Hii huwafanya wapiganie kumiliki nyumba za kupangisha ili waachane kabisa na ajira yao.
Tatu; kipaji.
Wapo wafanyakazi ambao hukwamishwa kukuza vipaji vyao kwa sababu ya kanuni na taratibu za ajira zao. Hii huwafanya wakose amani katika mioyo yao.
Hii inakuwa ni KWANINI KUBWA kwao ya kuwasukuma kumiliki nyumba za kupangisha ili watumie vyema uwezo ulio ndani yao kutoa thamani kubwa mno kwa wengine.
Nne; mamlaka na utawala.
Wapo wafanyakazi ambao wana uwezo mkubwa wa kutawala na kuwaongoza wengine.
Na wana ndoto hiyo ya kutawala wengine wakiamini watakuwa wamefanya kusudi la kuwatumikia wananchi wao. Hawa nao wanaweza kuonekana hawana maana mbele zao wananchi kama watakuwa maskini.
Hivyo huamua kumiliki nyumba za kupangisha ili waweze kupata kipato cha kuweza kufikia maono yao. Hii kwao inakuwa ni KWANINI KUBWA ya kuwafanya wasipate usingizi kabisa.
Tano; Utajiri mkubwa wa kifedha.
Kuna kundi lingine ambalo husukumwa zaidi na kutaka kuwa matajiri na kuweza kufanya mambo mema wayatakayo. Hawataki kuomba omba.
Wanataka kukusanya pesa nyingi sana kiasi kwamba wataweza kufanya majaribio ya kuhamia sayari zingine.
Kwa makundi haya matano, ni lazima upate KWANINI KUBWA yako kama kweli unahitaji kupata mafanikio makubwa kwenye nyumba za kupangisha.
Hata uwe na shahada (digrii) tano zinahusu fedha na uwekezaji kwenye viwanja na nyumba, kama hauna kwanini kubwa huwezi kumiliki nyumba za kupangisha za kuweza kukufanya upate mafanikio makubwa.
Hata uwe mbobezi wa viwango vya kimataifa kwenye majengo ya kupangisha kama hauna KWANINI KUBWA, huwezi kupata mafanikio makubwa kupitia nyumba za kupangisha.
Karibu unishirikishe lengo lako kuu la kuamua kustaafu mapema kupitia majengo ya kupangisha. Tumia namba ya WhatsApp au jiunge na kundi langu la Telegramu hapo chini ili uwe karibu zaidi na mimi.
Siku nyingine nitamalizia kukushirikisha na mambo matatu yaliyobaki nayo ni; malengo makubwa, mifumo na mbinu bora sana na tabia za kiuwekezaji.
Mwandishi,
Aliko Musa.