Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 380
- 550
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika kesi hii ya Lwakatare ninachokiona ni matumizi mabaya ya sheria na wale waliombakizia kesi Lwakatare wanastarehe na kufurahi kuona Lwakatare anaenda kuishi gerezanialidai Profesa Safari.
Mipango ya kigaidi haiwezi kupangwa na mtu mmoja. Wote waliohusika wataenda kuozea gerezani.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Kama nilivyokwishaeleza hapo mwanzo sheria nzima ni ambiguity inatumika kwa matakwa ya wanaoitumia kwa muda huo lakini si kwa kuleta piece and tranquility jambo ambalo ni msingi wa sheria za nchilwakatare na ludovick wanakabiliwa na mashtaka yafuatayo;
1.kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya adhabu sura ya 16. Ya mwaka 2002, washtakiwa walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru msacky kinyume na sheria kanuni na taratibu.
2.washtakiwa kwa pamoja walikula njama ya kufanya kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria cha 24.2 cha sheria dhidi ya ugaidi.
3.washtakiwa kwa pamoja walishirikiana kupanga njama za utekaji nyara dhidi ya msacky kinyume na sheria inayopinga ugaidi.
(washtakiwa walifanya mkutano wa vitendo vya kigaidi).kwamba washtakiwa walipanga na kushiriki mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara dhidi ya msacky.
4. Lwakatare peke yake anakabiliwa na shtaka la nne la kuhamasisha vitendo vya ugaidi, na kwamba siku hiyo ya tukio lwakatare alitumia nyumba yake kama mwenye nyumba, akijua, aliruhusu mkutano kati yake na ludovick ufanyike katika nyumba yake kwa lengo la kuhamasisha vitendo vya ugaidi dhidi ya msacky.
Tunatarajia sheria itafuatwa na haki itatendeka ili kukomesha vitendo kama hivi katika jamii iliyostaarabika ya watanzania