Hii ndiyo Siri Kubwa ya Yanga SC Kung'ang'ania Kuvalia Jezi yao Nyeusi tu na kuwa tayari hata Kulipa Faini kila mara

Cognizant

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
626
Reaction score
1,409
Baada ya Mganga wao Hatari wa Kienyeji kupelekewa Jezi zote hasa kabla ya kwenda nchini Tunisia Jezi pekee iliyokubalika kwa Dua, Mizimu, Kafara na Uchawi ni ya Rangi Nyeusi yenye Saini za Waliokuwa Wachezaji Nyota na Mahiri wa Klabu hiyo.

Hivyo basi baada ya Mganga wao Hatari kulijua hilo aliamua Kuisomea Dua Kali Jezi hiyo Nyeusi iitwayo KUNUTI ambayo inazuia Watu Wabaya wote na Mabaya yote yanayoelekezewa Kwao.

Athari pekee ambayo itaikumba na tayari imeshaanza Kuikumba Klabu hiyo ni kwamba tayari hata Wachezaji wa Yanga SC wameshaanza Kuathirika Kisaikolojia ambako wasipovalia Jezi Nyeusi wanakuwa Wanyonge ila wakivalia Jezi Nyeusi huwa Wachangamfu na wenye Morali ya hali ya Juu mno kwani hata Wao Wachezaji wa Yanga SC wameshaaminishwa kuwa ndiyo Jezi yenye Bahati / Nyota ya Ushindi Kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…