Waungwana habari zenu naamini mko swalama salimini,leo nimeamua kuuleta ukweli juu ya masuperstaa wakubwa hapa bongo yaani wasanii wenye nafasi zao kubwa katika ladha ya bongo(bongoflavour) na wasanii wenyewe ni huyu DIamond wa tandale from kigoma na Ali salehe kiba wakiwa wote from kigoma mkoa.Huwa kunakuwa na mitazamo mingi sana ya kiushabiki inayotolewa na wadau mbalimbali wakilenga kuwatofautisha hawa wasanii lakini waandishi wengi wanajikita katika ile nani anapendezwa naye.
Kwanza,kiukweli mimi ninaamini diamond ameufikisha muziki wa bongo mbali sana na kutangaza taifa letu na hivyo utakuwa humtendei haki ukikubali uwezo wake na hata kuweza kumtunuku ufalme wa mziki wa bongo(mafanikio) ukitofautisha na braza alikiba.
Unapozungumzia wasanii hawa ili kupata sifa zao kirahisi ni sawa na kuwafananisha na wachezaji,RONALDO cr7 na MESSI,Alikiba ana uweza muziki nikimaanisha muziki ni kutoka ndani ya damu kabisa na hata ukifatilia kipindi anaanza enzi hizo alikuwa anafanya muziki kama hobby tuu alimradi asizike kipaji,alikiba amekulia kwenye maisha ya kidini kidogo na hivyo kumfanya kuwa na hofu kidogo kimwenendo chunguza hata jinsi the way anaishi,jamaa sio mtu wa kiki nyingi sana wala skendo za kumwaga radhi hata watu wote wakajua,jamaa hata uvaaji wake hapa wote mtaamini huwa anavaa kimaadili kidogo kiasi kwamba kama humfahamu ukioneshwa kuwa ni msanii huwezi kuamini,jamaa havai mahereni mara kuvaa misalaba mara kuweka vipini puani mara kupaka marangi kichwani au mdomoni so inshu zima ni upande wa maadili zaidi yaani ile hofu ya kujiharibia haiba kwa watu ndio kitu alichonacho huyu jamaa,ndio maana kuna muda anaonekana mbinafsi kisa hapendi mikiki na miskendo ya kujichafua.
Lakini diamond platnumz,jamaa ana kipaji cha ajabu sana,ana mziki mzuri sana ila yeye kajikita katika muziki biashara kiasi kwamba hata iweje hawezikufaya show ya watu kumi hata iweje na inaonesha yeye mziki ulikuja baada ya zile harakati za kujitatua na hali ngumu ya maisha kule tandale enzi zile,lakini diamond hana haiba nzuri kabisa hebu angalia skendo zake sometimes ni kujitakia tuu kutaka kila kitu kiwe ni sehemu ya kujiongezea habari au umaarufu(kiki) mitaani,Jamaa kakosa kitu muhimu kimoja tuu ile haiba binafsi maana utamuona na mahereni,mikufu mingi,mara majeans yamechanika mapajani,mara rangi midomoni na kwenye nywele tena afadhali kwenye nywele shortly jamaa yupo nje ya kimaadili,kwani ukiwa msanii lazma uvae mlegezo?,vipi PROFESSA J,NIKK WA PILI,JAY Z huko mambele mbona wako humble tu.
Kuna muda huwa nawaza labda pengine ni haya masuala ya malezi kwa kuwa jamaa kalelewa na mzazi mmoja cha kwanza,na ukizingatia mama aliyemlea nae ndio hivyo MIRUKO na usikute ndio sababu ya baba diamond kupita kushoto(wanaume wanajitambua ukiona kamwaga mwanamke kuna tatizo katika akili ya huyo mwanamke)tofauti na kiba ambaye kalelewa na wazazi wote wawili.Lakini yote katika yote ni vema mtu ukiwa na nafasi kubwa kama mfano katikajamii,jamii ikikuheshimu basi huna budi kujiheshimu.Kwahiyo diamond kaka jiheshimu unao muda wa kubadilika licha ya yote.all in all mimi ni miongoni mwa tunaopenda muziki wa diamond na lengo la uzi kubadilshana.
Ahsante,
View attachment 804801View attachment 804802