Hii ndo namna pekee ya kuwasaidia vijana wa Kitanzania. Soma utakuja kunishukuru

Hii ndo namna pekee ya kuwasaidia vijana wa Kitanzania. Soma utakuja kunishukuru

Jebel

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2021
Posts
347
Reaction score
2,325
Habarini Waungwana!

Natumaini Mungu anaendelea kumjalia kila mmoja wetu kadiri ya mapenzi yake.

Utangulizi
Kwanza naomba nianze kwa kusema kwamba vijana wengi wa KiTanzania ni wachakarikaji, wapambanaji, wapiganaji tofauti na vijana katika nchi nyingi sana ambazo nimewahi kutembelea au kufika. Ni kweli kwamba wapo wategeaji wachache sana na wapo wengine ambao wanatamani kuwa wapambanaji lakini wanakosa kung’amua fursa sahihi ya kupambania. Kimsingi ili upambane ni lazima ujue cha kupambana nacho! Ukitaka kuniamini nachokisema juu ya vijana wa KiTanzania, jaribu kutembelea sehemu zenye fursa fulani ya kupata riziki hapo ndo utakapoamini maneno yangu.

Leo nimeona nitoe idea ambayo naamini vema kwa namna moja ama nyingine inaweza kuwasaidia vijana kadhaa, kama 10 au 20 au 50 au 100 watasaidiwa na idea hii, basi sifa na utukufu vitamrudia Mwenyezi Mungu aliye juu ya vyote.

WAZO: BIASHARA YA SAMAKI AINA YA DEGERE

1. Ufafanuzi
Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisheria kusafirishwa na kuuzwa. Samaki hawa huwa kwa kiasi kikubwa wananuliwa na watu ambao wanaenda kupika majumbani na kwenye migahawa.

2. Sehemu ya kufanyia biashara hii
Kwa uzoefu wangu sehemu sahihi ambayo biashara hii itaweza kukutoa haraka sana kama ukiifanyia katika jiji la Mwanza. Kuna sababu juu mbili za kupendekeza jijini Mwanza
a) Upatikanaji wa bidhaa samaki kwa urahisi na wingi
b) Soko la uhakika yaani wateja wengi kutokana na idadi ya wakazi kuwa wengi katika jiji hili.
c) Gharama ya maisha katika jiji la Mwanza ni ndogo sana kuanzia chumba cha kupanga hadi chakula.

3. Chimbo la bidhaa samaki degere
Samaki hawa unaweza kuwa unawanunua katika mialo ya pale pale Mwanza mjini, mwalo maarufu sana ni Mkuyuni kwa Mswahili, hapa ni karibu sana na njia panda ya kwenda Butimba. Changamoto ya mwalo huu au ununuzi wa samaki katika mialo hii ya mjini ni competition kubwa ya wanunuaji hasa wanawake, kama wewe siyo mzoefu lazima utakimbia na kuachana kabisa na biashara hii.
Ushauri: sehemu sahihi ya kununua samaki hawa kwa bei ya chini, bila mashindano na faida kupata kubwa sana ni kwenda kisiwani.
-Hapa napendekeza zaidi kisiwa cha Bwiro. Huku utapata samaki wengi, wazuri, bei nzuri, na utapiga faida kubwa sana ukiwafikisha Mwanza mjini.

4. Namna ya kufika na sehemu ya kulala
Kutokea Mwanza mjini hadi Bwiro nauli ni 4000-5000 tu, boat au meli. Kuna boat 3; Nyachijanja, Umia Ujae kubwa na Umia Ujae ndogo. Zinatoka Kirumba saa 4/5 asubuhi kila siku. Ni mda wa masaa3 na nusu hadi 5 kulingana na hali ya hewa ya siku hiyo. Ukifika kule guest ni kuanzia shilling 2000-4000. Kule ningeshauri ufikie guest ya Kasemele bei ya 4000 kwa mgeni ila ukishakuwa mwenyeji ni 3000. Ni guest nzuri, safi, vitanda safi 5/6 chuma, mashuka safi, maji masaa24/7. Ni pazuri sana.

5. Mtaji
Biashara hii mtu yeyote anaweza kuifanya kwani mtaji wa elfu hamsini 50,000/= unatosha kabisa kwa kuanzia na baada ya kuuza utashangaa faida utakayoipata. Samaki hawa bei yake kwa kule kisiwani ni kuanzia 1000 au pengine kama wamepatikana kwa wingi unanunu samaki 3 kwa 2000. Ukiwa na 50elfu unapata mzigo mzuri sana wa kutosha na ukishaaminika hata kama huna hela utapewa samaki na ukirudi unalipa.

6. Sehemu ya kuuzia
Kwa Mwanza mjini sehemu yoyote utakayopanga samaki hawa hasa pembezoni mwa barabara lazima samaki watanunuliwa na wataisha bila shida yoyote. Ningeshauri kwa mtu atajayekuwa interested afanye kwanza mzunguko kwa pale mjini na viunga vyake kama Nyegezi, Nyashishi, Buhongwa na maeneo mengine aone population na namna wengine wanavyouza; bei na utokaji.
Hata kama huna mtaji wa kulipia meza katika masoko ya samaki unaweza kuanza na hii ya kupanga pembezoni mwa barabara na baadaye unaweza kuanza kulipia meza kwa kuungana na wengine.

7. Faida yake
Faida mama ya samaki hawa siyo mnofu utakaouza bali ndani yake kuna “kidude” kinaitwa “bondo “. Kinakuwa kama sehemu ya utumbo lakini ni very valuable kwani hiki kidude ndicho kinachotumika kutengeneza hizi nyuzi za kushona binadamu ambazo hazitolewi bali zinayeyeka zenyewe, hasa operation ya sehemu ambazo ni sensitive. Kumbe utagundua kwamba samaki ambaye umemununua shilling 3000 kule kisiwani unaweza kumuuza 5000 mjini Mwanza na bondo utakalotoa ukaliuza shilling 2000 au 1500 au 1000 au zaidi kutegemeana na size yake. Kwa hiyo utagundua kuwa utapiga faida sehemu mbili, kwanza kwa kumuuza samaki mwenyewe na pili kwa kuuza bondo lake. Kwa ufupi kama samaki umewanunua kisiwani ni lazima upate faida nzuri tu ukiwafikisha mjini.

JE, UMESHAWAHI KUJIULIZA NI KWANINI KILA KUKICHA WATU WANAJENGA MAJUMBA PAMOJA NA HALI KUWA NGUMU? BASI HAYA NDO MADINI YA KUSOMA ILI NAWE UFANIKIWE.

8. Changamoto zake
Biashara hii kama zilivyobiashara zote nayo inachangamoto zake japo siyo kubwa sana. Changamoto ambazo nitazigusia na kutoa ushauri ni mbili:

a) Usafiri wa majini. Binafsi kilichonifanya niache kufanya biashara hii pamoja na faida yake kuwa nzuri ni baada ya familia yangu kutopenda niendelee kufanya biashara ya kusafiri majini. Binafsi natokea mkoa ambao hakuna ziwa karibu kwa hiyo wazazi na ndugu zangu walikuwa na hofu sana wanaposikia najishughulisha na biashara ya kwenda kusafiri majini mara kwa mara. Hata aliyekuwa mchumba wangu(kwa sasa mke wangu…nampenda sana) alikuwa hapendi sana mimi kwenda majini japo hakuwahi kunikataza.

Ushauri, usafiri wa majini naweza kusema is more safe kuliko aina nyingine yoyote ya usafiri kuwahi kutokea. Kwa sasa kwa sababu ya maendeleo ya sayansi ya mawasiliano hata ikitokea shida yoyote msaada unafika mapema tofauti na siku za nyuma. Majini kwa sasa mtandao unasoma 3G, lakini pia kila boat kuwa kuna maboya kwa kila abiria.

b) Changamoto ya pili ni usumbufu wa maliasili kwani samaki hawa kama nilivyosema mwanzoni hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa. Hawa huwa wakiwakamata samaki na wewe usiongee vizuri, yaani ukaanza ubishi na ugalalizi basi wanaweza kuchukua na kukufirisi mzigo wote. Hakuna kifungo wala faini bali wanachukua samaki tu. Binafsi nimewahi kukamatwa sana nao lakini ni rahisi sana kuongea nao na bahati nzuri wanahitaji elfu 5 hadi elfu 10 na maisha yanaendelea. Ushauri, ukianza biashara hii, jitahidi kuwafahamu kwani mda mwingi wanakuwa kivukoni, jenga nao urafiki, wambie ukweli juu ya uchakarikaji wako, wape kidogo; biashara utafanya vizuri sana.
Changamoto hizi zote kwa mtu ambaye yupo serious kweli ameamua kuingia biasharani basi ataweza kupambana nazo vema.

Ushauri na hitimisho
Kisiwani maisha ni ya kipekee sana, kutokana na mzunguko mkubwa wa pesa hasa wakati wa giza shauri ya wanunuzi wa dagaa kutoka maeneo tofauti tofauti ya nchi kuingia kule kununua dagaa, basi mabinti nao wanatumia fursa hii vema. Kumbe inawezekana ukaenda na mtaji lakini usipokuwa makini nao unaweza kurudi kwa kuomba lift ya boat. Kuwa makini sana ukiwa kule.

Ukiwa serious sana na biashara hii, baada ya mda mfupi sana unaweza kukusanya pesa ya kutosha na ukaweza kupiga hatua kubwa sana kimaisha na baadaye UTAKUJA kunishukuru.

Mwisho, kama hukubahatika kusoma uzi mwingine niliiandika “KAMA UNA MTAJI FANYA BIASHARA HII UTAKUJA KUNISHUKURU” unaweza kuutafuta na ukausoma.

Kwa maswali na ufafanuzi zaidi usisite kuuliza kwenye section ya comment. Kwa sababu ya majukumu mengi nashindwa kujibu kila mtu inbox japo unaweza kutuma text nitajitahidi kujibu.

ASANTENI NI MUNGU AZIDI KUWABARIKI.

“Aquila non capit muscas”.
 
Huwa nikiona neno "utakuja kunishukuru" najua ndio wale wazee wa fursa

USSR
 
Huwa nikiona neno "utakuja kunishukuru" najua ndio wale wazee wa fursa


USSR

Umesoma mzee wangu? Mimi siyo Qnet wala sina undugu nao, nawachukia kuliko kitu chochote. Soma ukiona harufu ya fursa nijuze nami nitaondoa uzi na sintakuja kupost tena kitu chochote JF. ASANTE USSR:
 
Hayo mabondo unayosemea, huko visiwani unapoenda kuchukulia hao samaki je utayakuta ndani ya samaki au wajanja nao wanayatoa kabla ya kuuza samaki?
 
hayo mabondo unayosemea, huko visiwani unapoenda kuchukulia hao samaki je utayakuta ndani ya samaki au wajanja nao wanayatoa kabla ya kuuza samaki?

Itategemea na bei inayotoa wewe mununuzi, unaweza kununua samaki akiwa na bondo kwa bei ya juu kidogo au akiwa ametolewa bondo na bei itapungua Maova
 
Shukran sana kwa kutupatia fursa. Tanzania kuna 'harakati'nyingi sana ila watu hawana taarifa sahihi.

Tukishapata taarifa kama hivi we subiri utaona mrejesho.
 
Aiseee kweli ukosefu wa ajira umefanya vijana tujue vitu vingi vya kiujasiriamali, nashukuru pia kuona vijana aina ya Jebel mkitushirikisha mambo kadha kwa kadha.
Bado nafanya uchambuzi wa fursa sahihi zaidi kwangu ili nijitumbukize huko mazima.
 
Habari kiongozi

Nina Swali dogo

Hao samaki ukiwachukua kisiwani huko mpaka uwalete mjini si wanakuwa wameshachina

Mfano mm nina mpango wa kwenda kuwauzia kisesa

Je, hawatafika wameharibika maana wanachukuliwa wabichi?
 
Mkuu asante kwa somo zuri, ila hapo kwenye bondo ungenifafanulia vizuri make kuna kipind nilikua ukerewe (kakukuru) pale hao degere kabla hujauziwa kwa bei nafuu wajuba wanaondoa kwanza bondo na wanakuuzia samaki asie na bondo au kwa bwiro ni tofauti.
 
Habari kiongoz
Nina Swali dogo
Hao samaki ukiwachukua kisiwani huko mpaka uwalete mjini si wanakuwa wameshachina
Mfano mm nina mpango wa kwenda kuwauzia kisesa

Je hawatafika wameharibika maana wanachukuliwa wabichi?

Salama ndugu, hii biashara nimefanya kwa mda na hili nalokwambia ni uhakika kabisa, samaki hawa hawaharibiki unachotakiwa kufanya ni kuwawekea mchanga na kuwaweka vema ndani ya mfuko wa gunia kisha kwenye boat unawaweka chini ili wasifikiwe na jua. Kisesa utawafikisha vema na nakwambia baada ya mwezi UTAKUJA hapa jamvini kutoa shukurani na ushuhuda. Kikubwa zingatia ushauri nilioutoa na kama utakuwa na Swazi jingine usisite kuniuliza ndugu.
 
Mkuu asante kwa somo zuri....ila hapo kwenye bondo ungenifafanulia vizuri make kuna kipind nilikua ukerewe (kakukuru) pale hao degere kabla hujauziwa kwa bei nafuu wajuba wanaondoa kwanza bondo na wanakuuzia samaki asie na bondo au kwa bwiro ni tofauti...

Kwa Bwiro hakuna utofauti sana, ukinunua degere mwenye bondo kwa 3000, maana yake ungemnunua 2000 bila bondo. Kwa hiyo ni vema ununue kwa 3000 kisha ukamuuze 4000 au 5000 mjini bila bondo na bondo uuze kati ya 1500-3000. Kikubwa ni hesabu yako, unawaangalia samaki kisha unawatathmini. Baada ya mda mfupi utakuwa mzoefu ndugu.
 
Kwanini iwe kisiwa cha Bwiro na si kisiwa kingine?

Naamini victoria kuna visiwa vingi vya wavuvi

Isije kuwa umewekeza huko migahawa, bar, lodge, mitumbwi nk. Unataka watu waelekee Bwiro.

Ikiwa sivyo, fursa ni nzuri na asante kuwashirikisha wadau
 
Mleta mada katumwa na watu wa mali asili. Ukubwa wa samaki hao ni haramu kuvuliwa na kuuzwa!
 
Mleta mada katumwa na watu wa mali asili. Ukubwa wa samaki hao ni haramu kuvuliwa na kuuzwa!
Ninavyowajuwa Wabongo sehemu yenye kupiga pesa hakupi password hata siku moja.

Yeye mwenyewe ameacha hiyo biashara baada ya kuona ni biashara kichaa.
Ukiamuwa kufanya biashara haram basi uza dawa za kukevya ujuwe moja.
 
Back
Top Bottom