Hii ndoto ina maana gani?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kuna kitu nimekiota leo ambacho bado natafakari Sipati majibu

Nimeota kuna baba moja ambaye alikuwa na watoto wengi saana na wote walikuwa wanakaa ndani ya nyumba moja.

Sasa kwa bahati mbaya nyumba ile ikaungua moto baba yule akatoka ndani ya nyumba ile mbio na kukimbia kuokoa maisha yake.

Kilicho ni shangaza baada ya Baba yule kutoka akafunga mlango ule kwa makusudi familia yake yote ikaungua kwa moto alafu akapona peke yake.

Nikabaki na shangaa kwanini huyu baba amefanya ivo. Baba mmoja kikongwe akatokea na kuniuliza je kama nimeona yote yaliyo tokea nikajibu ndio cha ajabu akacheka na kunijibu kuwa nilicho kiona ndicho kinakwenda kutokea duniani.

Hii ndoto najaribu kutafakari sipati maana yake.
 
Mkuu kwenu mna maagano ya kichawi? Mizimu je? Vipi ukoo wenu ni WA kuchifu? Ni mara ngp unaota ndoto za ivo? Tuanzie apo kwan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…