Mungu peke yake ndiye hutafsiri ndoto. Na ili akutafusirie, omba kuelewa maana ya hiyo ndoto.
Lakini jiulize. Sehemu unayoishi ina mto? Ulishawahi kuishi sehemu yenye mto? Nauliza haya kwa sababu ndoto nyingi lazima zisimamie maeneo, maeneo ambayo yalianzisha tendo lolote ovu au zuri unalolipata maishani.
Kama unaota ukiwa kwenye maji, inawezekana kabisa kuna vipingamizi kwenye maisha vya kukuzamisha. Ili kujua hili pingamizi lilipoanzia au wakati gani, basi inabidi utambue huo mto upo maeneo yapi.
Kitabu cha Ayubu au Job 33:15-16 kinasema. 15 Mungu huongea na watu katika ndoto na maono, wakati wa usingizi mzito unapowavamia, 16 wanaposinzia vitandani mwao. Hapo huwafungulia watu masikio yao; huwatia hofu kwa maonyo yake.