Hii ngoma ya Al Hilal na Yanga bado ngumu

Hii ngoma ya Al Hilal na Yanga bado ngumu

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kama mpira ni uchawi basi tuseme Yanga bye bye, lakini Kama siyo uchawi ni uwezo wa timu na mbinu za makocha basi hii mechi ya Yanga dhidi ya Al Hilal bado ngumu sana tena sana.

Kama uliangalia ile mechi ya kwanza vizuri Yanga inaonyesha ina washambuliaji wazuri zaidi ya Al Hilal na huku ikiwa Yanga Al Hilal watatumia mpira wa kushambulia Yanga zaidi kuliko kuzuia hakika watatolewa.

Kama watazuia na kutumia ma contre attacking itakuwa vigumu kwa Yanga kupata matokeo. Ila wakitumia hii mbinu ya kuweka viungo wengi katikati na kuzalisha ma shuti ya mbali hawa Al Hilal wanaweza kutolewa.

Ila ni macho yetu!
 
Kama mpira ni uchawi basi tuseme yanga bye bye
Lakini Kama sio uchawi ni uwezo wa timu na tastics za makocha
Basi hii mechi ya yanga vs al hilal bado ngumu saana tena saana
Kama ulicheki ile mechi ya kwanza vizuri yanga inaonyesha ina washambuliaji wazuri zaidi ya al hilal na uku ikiwa yanga al hilal watatumia mpira wa kushambulia yanga zaidi kuliko kuzuia hakika watatolewa
Kama watazuia na kutumia ma contre attacking itakuwa vigumu kwa yanga kupata matokeo
Ila wakitumia hii tastic ya kuweka viungo wengi katikati na kuzalisha ma shoot ya mbali hawa al hilal wanaweza kutolewa

Ila ni macho yetu
Huu sasa ndiyo uchambuzi.
 
Yanga hii naiamini 42 unbeaten games bado inatubeba sana

Kazi kubwa tuwaachie benchi la ufundi
Yanga watumie Video ya game iliopita kujikosoa makosa na mapungufu tuliyokua nayo

Wale ni wepesi sana kwetu kama hawatafanya figisu naiona Yanga yangu hiyooo katika makundi

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Umeandika vizuri ila Mpira wa Africa hauko Kama ulivyoandika hapa.Mara nyingi mashindano ya kiafrika kila mtu anashinda kwake.Ni ngumu kupindua meza ugenini,labda tu uwe mzembe na kudharau mechi km ile Simba na Galaxy.

Hawa Al hilal hawajaidharau hii gemu yao na yanga.Ibenge anajua yanga Ni hatari na watakuja na nguvu zote maana hawana Cha kupoteza,kwao (yanga) ili wafuzu lazima waweke mpira wavuni.Suluhu ya 0-0 yanga anatoka,so yanga wataenda na mentality ya kutafuta goli,na hapo ibenge ndipo atakapowaadhibu

Kwangu mimi,hata yanga angeshinda moja bill,bado kazi ingekuwa ni nzito Sana kule Khartoum,sembuse matokeo ya 1-1. Wacha tusubiri hiyo jumapili!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kauli ya ibenge baada ya gemu ya Dar er salaam Kuisha

"Nilijua yanga Ni timu Bora,ila hatukujua wana wachezaji Bora kiasi hiki.Kabla hatujaondoka Sudan kuja Dar es salaam mchezaji ambaye nilikuwa na mashaka naye zaidi ni Azizi ki.

Wakati tupo halftime kwenye chumba Cha kubadilishia nguo niliwaambia wachezaji kwamba yanga wataingia kwa Kasi kutafuta goli na endapo watapata goli itakuwa rahisi kwetu kupata goli maana akili ya yanga itakuwa kutufunga goli la pili ili mechi waimalize Dar es salaam.Kwa mentality hiyo wakipata goli,wakati timu nzima wanakuja kutushambulia sisi ndiyo tutafunguka kwa wings za pembeni kwenda kuwaadhibu.Kiukweli nimeumia na matokeo ya draw maana tulikuwa tuna uwezo wa kupata ushindi na kuturahishia kazi Khartoum"

Full time tukaona game plan ya ibenge imework na wakafanikiwa kutoka na draw Dar.So yanga kusema Al hilal walikuwa wepesi na kwao wanafungika Sidhani Kama Ni Kauli sahihi ya kimchezo,wakati wao Al hilal wanaona game plan ya ugenini imefanya vizuri

Ila lolote linaweza kutokea maana mpira Ni mchezo wa wazi,tusubiri tuone!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika vizuri ila Mpira wa Africa hauko Kama ulivyoandika hapa.Mara nyingi mashindano ya kiafrika kila mtu anashinda kwake.Ni ngumu kupindua meza ugenini,labda tu uwe mzembe na kudharau mechi km ile Simba na Galaxy.

Hawa Al hilal hawajaidharau hii gemu yao na yanga.Ibenge anajua yanga Ni hatari na watakuja na nguvu zote maana hawana Cha kupoteza,kwao (yanga) ili wafuzu lazima waweke mpira wavuni.Suluhu ya 0-0 yanga anatoka,so yanga wataenda na mentality ya kutafuta goli,na hapo ibenge ndipo atakapowaadhibu

Kwangu mimi,hata yanga angeshinda moja bill,bado kazi ingekuwa ni nzito Sana kule Khartoum,sembuse matokeo ya 1-1. Wacha tusubiri hiyo jumapili!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Hi ni jumapili au jumamos ? Mbna unatuchanganya mzee !!!
 
Yanga hii naiamini 42 unbeaten games bado inatubeba sana

Kazi kubwa tuwaachie benchi la ufundi
Yanga watumie Video ya game iliopita kujikosoa makosa na mapungufu tuliyokua nayo

Wale ni wepesi sana kwetu kama hawatafanya figisu naiona Yanga yangu hiyooo katika makundi

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Fuatilia na rekodi za al hilal kwenye game zake 42 ilikuwaje!?

Kama kumbu kumbu zangu zipo vzr kwenye hizo 42 games yanga hajafungwa lkn kavuna point chache, 106 km sikosei out 126 huku al hilal kafungwa moja ila kavuna point 114 out of 126. Kwenye hizo game yanga kashinda goli 60+ kafungwa goli nyingi wakati al hilal kashinda goli 88 kafungwa 11 tu. Overall performance kwenye hizo 42 games ni 83% Yanga kwa 94% al hilal usisahau al hilal anacheza ligi ya 8 kwa ubora afrika wakati yanga akiwa ligi ya 11 kwa ubora afrika.

Hii inakuonesha (statistically) al hilal ni bora zaidi mara dufu ya yanga ukijumlisha na faida ya goli la ugenini na kumalizia uwanja wa nyumbani utajionea mwenyewe.

Kwa lipe vibe la omdurman Kazi mnayo mwanawane [emoji16]
 
Kama mpira ni uchawi basi tuseme Yanga bye bye, lakini Kama siyo uchawi ni uwezo wa timu na mbinu za makocha basi hii mechi ya Yanga dhidi ya Al Hilal bado ngumu sana tena sana.

Kama uliangalia ile mechi ya kwanza vizuri Yanga inaonyesha ina washambuliaji wazuri zaidi ya Al Hilal na huku ikiwa Yanga Al Hilal watatumia mpira wa kushambulia Yanga zaidi kuliko kuzuia hakika watatolewa.

Kama watazuia na kutumia ma contre attacking itakuwa vigumu kwa Yanga kupata matokeo. Ila wakitumia hii mbinu ya kuweka viungo wengi katikati na kuzalisha ma shuti ya mbali hawa Al Hilal wanaweza kutolewa.

Ila ni macho yetu!
ila ni macho yetu😓
 
Hamna haja ya kuhangaika, atae tuua io game ni mayele wala sio al hilal, mechi ya kwanza ilibidi aondoke na kiatu chake pale taifa, nafasi mbili za wazi alipoteza akaja kufunga goal gumu. io mechi akitupia goal mbili tu temepita maana naona na sisi lazima turuhusu bao.
 
Kama mpira ni uchawi basi tuseme Yanga bye bye, lakini Kama siyo uchawi ni uwezo wa timu na mbinu za makocha basi hii mechi ya Yanga dhidi ya Al Hilal bado ngumu sana tena sana.

Kama uliangalia ile mechi ya kwanza vizuri Yanga inaonyesha ina washambuliaji wazuri zaidi ya Al Hilal na huku ikiwa Yanga Al Hilal watatumia mpira wa kushambulia Yanga zaidi kuliko kuzuia hakika watatolewa.

Kama watazuia na kutumia ma contre attacking itakuwa vigumu kwa Yanga kupata matokeo. Ila wakitumia hii mbinu ya kuweka viungo wengi katikati na kuzalisha ma shuti ya mbali hawa Al Hilal wanaweza kutolewa.

Ila ni macho yetu!
Mkuu huoni kama kuna haja ya kupumzika sasa na kusubiri game ipigwe?

Maana kabla ya game ya nyumbani uliwatangazia watu kuwa Yanga atashinda magoli 3 ikawa tofauti

Kuanzia hapo umekuwa mpiga Ramli wa club, haipiti siku bila kuanzisha Uzi wa Yanga Vs Al hilal

Unabadirisha tu headings ila maudhui yote ya thread zako ni zile zile
Yanga atawashangaza
Yanga anaenda kupindua meza
Yanga ana wachezaji Bora kuliko Al hilal
Yanga..... Al hilal
Yanga ....... Al hilal

Sisi kama wasomi wa thread zako tunasema tushakubariana nawewe kuwa Yanga anaenda kushinda huko Sudan na kama hutojali basi badirisha aina ya nyizi

Anzisha ata Thread za kuandaa mapokezi ya club baada ya kushuka uwanja wa ndege wa Nyerere

Tupe ratiba ya bus la wazi litapita barabara gani ili sie tujipange mstari barabarani tukiwapungia mikono mashujaa wetu
 
Back
Top Bottom